Busara itumike mtoto aliyeshawishiwa kukojolea msaafu!

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
Imagine una oga kwenye bafu la passport size akaja mtoto akachukua nguo zako pamoja na taulo,ukatoka nje uchi wa mnyama ukaanza kumkimbiza,nani ataonekana chizi?? Hii scenario inafanana na sakata la mtoto aliyeshawishiwa kukojolea msaafu.

Hii issue ni ndogo sana tena imefanywa na mtoto ambaye yuko katika maturity age.

BUSARA NA HEKIMA ITUMIKE kwa huyu mtoto,kama busara ilivyotumika kwa waliokataa kuhesabiwa sensa ambao walivunja sheria. au busara ilivyotumika kumuachia DIBAGULA aliyekashifu wakiristo kuwa YESU SIO MUNGU, au busara ilivyotumika kumuachia kiongozi wa UAMSHO.

Busara itumike zaidi na huyo mtoto aachiwe huru la sivyo panaweza kuchimbika na kusababisha amani na utulivu kutoweka.
 
Ni matumaini yangu kuwa busara itatumika kwenye hili sakata la mtoto aliyeshawishiwa kukojolea msaafu.
 
Kuweka mambo sawa ni kuwa hakukuwa na ushawishi wa mtu. Ni watoto wanaojuana na wakakutana mmoja akitoka madrasa. Katika kuongea ikatokea ubishi wa kidlni. Mtoto wa kiislamu alimuhakikishia mtoto wa klkristo kuwa kitabu hiki ni kitakatifu na ukienda kinyume utakuwa chizi. Mtoto wa kikristo akabisha ndo kale kakamwambia nakiweka chini ukojolee na hakika sasa hivi utakuwa chizi. Jamaa akakojolea na hakikutokea chochote. Jamaa kuona hivyo akaenda kumweleza mwalimu wa madrasa na zogo likaendelea. Hakuna mshawishi wa nje hapo. Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom