Buriani Sajini Kassim Said Mapili

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Mapili wakati akiwa amelazwa Muhimbili.jpg

“KIFO oooh kifoo, kifooo kifoooo, kifo hakina huruma!” Naam. Ndivyo alivyoimba marehemu Ramazan Mtoro Ongalla ‘Dk. Remmy’ wakati akiwa na bendi yake ya Super Matimila ‘Wana Bongo Beats’ akiomboleza kuhusu ‘kifo’, Fikra Pevu inaripoti.

Kweli kifo hakina huruma, kwa sababu kinaweza kumchukua yule umpendaye katika wakati ambao bado unamhitaji.

Katika albamu yao ya Nippon Banzai ya mwaka 1994, Zaiko Langa Langa ‘Nkolo Mboka’ wanasema ‘Liwa yo Moyibi’, yaani‘Wewe kifo ni mwizi’! Hakika kifo ni mwizi kwa sababu kinatokea bila taarifa, hakipigi hodi, kinashambulia na kuwaacha watu wakiwa na majonzi na mpendwa wao.

Hakika ndivyo ilivyotokea kwa mkongwe wa muziki nchini Tanzania, al-marhum Kassim Said Mapili (79), ambaye amefikwa na mauti Februari 24, 2016 akiwa amelala mwenyewe nyumbani kwake maeneo ya Tabata TIOT jijini Dar es Salaam, tena baada ya kurejea kutoka kuangalia mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Arsenal na Barcelona.
ZAIDI HAPA...
 
Inna Lillahi Wainna Lillahi Raajurun!!! MUNGU Msamehe Dhambi Zake Na Mpe Makazi Mema!!!!
 
Back
Top Bottom