Buriani rafiki yangu

KING ASSENGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
929
Reaction score
1,501
kijana mwenye jinsia mbili alipata shida ya kibofu cha mkojo na kufanyiwa surgery

Lakini hali yake haikutengamaa bali ndio ikazidi kuwa mbaya sana sana .
Sasa jana kanitumia meseji watsap.

Kaka asante kwa kuwa rafiki bora zaidi ya rafiki , ndugu zaidi ya ndugu
Nilifurahia sana kampani yako kwenye maisha yangu kwa muda tuliofahamiana . Ulinipa tabasamu na kidogo kupata mwanga wa kuishi bila kujutia nilivyoumbika na pia kupata faraja na matumaini makubwa kiroho . Japo kuwa ulinifanya nipende kuishi

Ila kwa sasa sina jinsi naondoka ninahuzuni . ila nikikumbuka tumaini la maisha ya uzima wa milele ulilonihubiria basi sina sababu ya kuhuzunika sana nimeshateseka sana na nikiwaza dunia isiyokubali nilivyoumbwa acha tu nipumzike kaka acha nipumzike . Kwaheri bro tutaonana kwenye uzima wa milele jitahidi uishi maisha uliyonihubiria tukutane huko siku moja.
Asante sana bro .

Hayo ndio maneno ya mwisho ya rafiki yangu kijana mwenye jinsia mbili.

Nilipiga simu haikupokelewa leo napigiwa simu naambiwa kijana hatunae tena , sijaweza kumuuliza hata yeye ni nani ila nisauti ya mwanamke mtu mzima alikuwa analia sana.
Nina huzuni sana , nitamisi sana meseji zake na ukaribu wake na mimi utani wa kutosha
Hakuna siku iliyopita bila kuongea na kuchat
R.i.p
 
kijana mwenye jinsia mbili alipata shida ya kibofu cha mkojo na kufanyiwa surgery

Lakini hali yake haikutengamaa bali ndio ikazidi kuwa mbaya sana sana .
Sasa jana kanitumia meseji watsap.
Pole sana kwa kuondokewa na mtu aliyethamini na kutambua uwepo wako. Ulimpa kitu kipya kwenye maisha yake ambacho ameondoka nacho.

Ushauri wake ni wa muhimu kuuzingatia.
 
Kifo daaa nakiogopa jamani .nawaza sana siki ghafla nikisepa je nitakuwa na uwezo wa kuwaona mnavyo uzunika na watakao nicheka ,kifo akina urumaaaa
 
Kifo daaa nakiogopa jamani .nawaza sana siki ghafla nikisepa je nitakuwa na uwezo wa kuwaona mnavyo uzunika na watakao nicheka ,kifo akina urumaaaa
Kuna jamaa kafa kifo kibaya sana kakanyagwa na DCM kichwa kime-bust, kuna ndugu yake mmoja nimemkuta mtoni analia vibaya sana nikasema huyu watu wakae nae karibu huyu atajitosa mtoni huyu
 
Nimepatwa na huruma na kusikitika Sana ghafla inaumiza na hayo maneno ya mwisho.
“Nipo kwenye maumivu makali Sana ila maumivu ya mwisho”
Sometimes hutakiwi kuwaza sana kuhusu kifo maana wote Safari yetu ni moja tu, kinachotutofautisha ni muda na siku ya kufa, na unaefikiri kwamba atawahi kufa ndie atakaechelewa kufa zaidi wote mnaweza mfe yeye akabaki
 
Ok.tuendelee kula bia ama?
Sungura (smartGin) 3 kubwa, Energy 1 Mo + 1 Bakhresa Azam mix na Ugoro na kipisi kimoja cha Bangi alafu zimua na Nyota (Sigara Kali) 1 saga na gomba pisi 1 choma na ubalozi mmoja wa Marekani, baada ya hapo kaa chini angalia mawingu na sikilizia mchemsho wa Figo zako na mapafu yanavyoenda kasi
 
Nakumbukaga uliwahi kupost humu kuhus huyo rafki mwenye Jinsia Mbili, Dah pole sana kw kuondokewa na Rafki yako Mkuu.
 
Sometimes hutakiwi kuwaza sana kuhusu kifo maana wote Safari yetu ni moja tu, kinachotutofautisha ni muda na siku ya kufa, na unaefikiri kwamba atawahi kufa ndie atakaechelewa kufa zaidi wote mnaweza mfe yeye akabaki
Mungu ni mwema sana ndugu yaani kuna vifo viwili nimevishuudia maishani mwangu nabaki kusema tumwache Mungu aitwe Mungu, kifo hakichagui na usijione mwamba au mzima sana aisee Mungu ana siri nyie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…