Buriani Pendo, Buriani mpenzi yangu

Pole sana mkuu,kifo tumeumbiwa sisi lakini hakizoeleki kamwe,cha muhimu na sisi tulio hai tujifanyie maandalizi ya siku yetu ikifika.......
Narudia tena kukupa pole mkuu
 
Naulazimisha mtima, uikubali hatima,
Mikono nikiachama , isilishikize tama ,
Japo chozi aandama , ujasiri najipima
Niseme si langu fungu , haujakubali mtima
Duniani si pa kwetu,sisi sote wapitaji
Moyo jipe wanakwetu, uvumilivu wako mtaji
Ndiye mfariji kwetu,hakika tavikwa taji
Hakika atakalo mola,binadamu hawezi zuia

Hakika Sasa yatosha,kufuru Mola utaja
Uchungu unapotosha,Sababu nyingi kutaja
Utulivu Sasa onesha,Lia panapo haja
Hakika atakalo Mola,binadamu hawezi zuia

Tuunge zetu nia,da Pendo muombea
Huku kitumainia, Siku moja kutania
Moyoni aminia,Dua zetu kutimia
Hakika atakalo mola,binadamu hawezi zuia
 
Sasa nimeamiani , kwa maulana twarudi
Tupo tuu mapitoni, upendo na uwe jadi
Saidia wa shidani, bila kujali idadi
Tumekosa nini Kifo , watuacha tu wakiwa

Kwake tuu maulana , ipo siku tutarudi
Ungetupa kuagana, kifo acha makusudi
Wabeba na wema sana, hata wale maridadi
Tumekosa nini kifo, watuacha tu wakiwa

Tunaamka alfajiri, na kuwasha telephoni
Twaambiwa yalojiri, kila siku ni msibani
Kifo achaga kiburi, kweli vilio huvioni
Tumekosa nini kifo , watuacha tu wakiwa [emoji24]
 
Pole Sana! Hongera kwa kuendeleza Sanaa ya ushairi!
 
Usihukumu maana hukumu ni juu ya Mungu peke yake, hakuna aliye mkamilifu katika hii dunia, Mungu wetu ni mwingi wa rehema na ni mwepesi wa kusamehe.
 
Unajifunza ushahiri au unaomboleza bruda
 
Samahani mkuu weka picha ya pendo tupate kumjua inawezekana ni ndug yangu
 
Haya, wewe ambaye sio mzinzi na muasherati umeshawahi kuuona huo ufalme?
 
Ndo mana huwa sifall in love NAOGOPA SANA KUMPOTEZA MTU NITAEMPENDA,sina hakika kama nitaweza kuvumilia uchungu wale..[emoji26][emoji26][emoji26][emoji26]
 
Ndo mana huwa sifall in love NAOGOPA SANA KUMPOTEZA MTU NITAEMPENDA,sina hakika kama nitaweza kuvumilia uchungu wale..[emoji26][emoji26][emoji26][emoji26]
Ni hatari sana , nyakat zote nzuri mlizokuwa nazo hazitafutika maishani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…