KING ASSENGA
JF-Expert Member
- Oct 8, 2016
- 929
- 1,500
Ur mourning or you are writing a poem?Ni juzi tulikuwako, kwa karamu yakufana
Ikiwa bathdei yako, Da! Pati ya kuagana
Ukanita Niko
AsanteMkuu pole sana
Bado haujakubali mtimaR.I.P[emoji24][emoji24][emoji24]Pendo .....mkuu ni safari yetu wote cha msingi tumuombee kheri kwa Mwenyezi Mungu ...
Hard timeUr mourning or you are writing a poem?
If ur mourning let wish ur soulmate Rest in Peace and if ur writing a poem you a good upcoming poet
Kuna sehemu umeona uasherati? Je kuwa wapenzi ni kufanya ngono , ni lugha sawa na alikuwa mchumba wangu tukiwa kabisa kwenye hatua ya kuingia kwenye ndoa, saratani ikakatisha safari yetuKwa hiyo Pendo amekufa akiwa katika status ya "uasherati".
Maana yake, kutokana na maelezo yako mwenyewe, wewe na marehemu mlikuwa hamjafunga ndoa, ila mlikuwa mnafanya "uasherati".
Kumbuka imeandikwa, "wazinzi na waasherati hawatauona Ufalme wa MUNGU kamwe".
Hakuna ajuaye siku ya kufa, hivyo basi ni vema sana kila aliye hai sasa hivi akajitahidi sana kuishi maisha ya usafi.
Usiogope kufa, bali, ogopa sana kufa ukiwa na DHAMBI!!!!!
Mwenye masikio na asikie.
Usihukumu usije ukahumiwa. Mpaka Pendo anaaga dunia hukuwa nae.... Swala la dhambi au mema ni lake na Mungu wake..... Sote hatuna ukamilifu mbele za MunguKwa hiyo Pendo amekufa akiwa katika status ya "uasherati".
Maana yake, kutokana na maelezo yako mwenyewe, wewe na marehemu mlikuwa hamjafunga ndoa, ila mlikuwa mnafanya "uasherati"...
Ni shairi ?? AuNi juzi tulikuwako, kwa karamu yakufana
Ikiwa bathdei yako, Da! Pati ya kuagana
Ukanita Niko ,Niko, Ati hatuta achana
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima
Siamini umeenda, hatutaonana tena
Yote tuliyoyatenda, hayatarudia tena
Popote tulipo kwenda, hatuwezi fika tena
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima
Siamini hutofika, kawaida kusalimu
Kwa utani tukicheka, Dah! Hilo tabasamu
Malengo yakipangika, mbeleni ndoa muhimu
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima
Ukapanga lake jina, la mtoto tukijaliwa
Kwa wakike Rihanna, wa kiume majaliwa
Ni mipango mingi sana, tulopanga maridhawa
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima
Umeniacha na kidonda, kutwa kucha ninakonda
Giza nene limetanda, moyo wangu ulipenda
Pendo leo umeenda, Najua sio kwa kupenda
Ni seme si langu fungu, haujakubali mtima
Moyo wajawa uchungu, hauijui hatima
Kwaheri', Mapenzi yangu, yamebakia yatima
Nisamehe sana Mungu, nizitoapo lawama
Niseme si langu fungu, haujakubali mtima
Ukaandika wosia, nifikie mazikoni
Eti niache kulia, siwezi huo mtihani
We ukiniandikia, pendo ulilia nini?
Mama yote kanitonya, kweli tulipendana
Nenda salama pendo, sisahau abadani
Ulinifunza upendo, uliozidi uzani
Umeacha pengo, pendo, Mpaka nije kwa manani
Kwaheri' mpenzi, Tutaonana baadae
[emoji120]Ulale salama Pendo, mwenzio akulilia,
Tungo zilojaa nondo, nyuma umemuachia,
Dhahiri kwa huu mwendo, machungu yamemjaa,
Mkafurahi pamoja, mbinguni mkutanapo.
Saratani saratani [emoji24]Ni shairi ?? Au