Buriani Jumbe, wanafiki tuwaone

Buriani Jumbe, wanafiki tuwaone

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
1471187162904.jpg


1
Hodi hodi kisimani, nina habari si nzuri,
Babu yetu Kigamboni, ameitwa na Qahari,
Jumbe si wa duniani, kaenda ile safari,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
2
Maisha yake huzuni, yajulikana dhahiri,
Katiwa kizuizini, ati si mtu mzuri,
Akatengwa Kigamboni, marufuku kusafiri,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
3
Alo yasema zamani, hadharani bila siri,
Kayatia kitabuni, mzee huyu jasiri,
MUUNGANO wa yakini, akafanya tafasiri,
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
4
Ikazuka tafarani, heri ikazaa shari,
Vyombo havielewani, vidau na manowari,
Kaskazi mkondoni, imechafuka bahari,
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
5
Katolewa mjengoni, urais ndo kwaheri,
Hakurudi na nyumbani, sasa miaka dahari,
Meli yake Magogoni, hakugusa Zanzibari,
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
6
"Kweli" itie shimoni, uichinje na buchari,
Ama itie motoni, jua tabaki ngangari,
Ipo siku tabaini, "kweli" ilivyo nawiri,
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
7
Turejee MAONI, ya katiba nashauri,
Mtaona naamini, Jumbe alivyoshamiri,
Miaka ni thelathini, mawazo bado ngunguri,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
8
Salamu toka kijani, tumepoteza hodari,
Kutoka serikalini, Jumbe kafa jasiri,
Tuwasute bila soni, zikome zao ghururi,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
9
Salamu za upinzani, Jumbe hakuwa hatari,
Haki alivyoamini, huletwa kwa kusubiri,
Ndio sababu jueni, isizuke halibari,
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
10
Wapinzani ahsanteni, na mtupe ikirari,
Siku gani hasa lini, mlikipanda kihori,
Mkenda kwake nyumbani, kumpa japo habari
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
11
Sasa niko tamatini, kufunga langu shairi,
Kuuliza natamani, mjibu pasi dosari
Alofia gerezani, vipi watamstiri?
Tutawona dhahiri, wanafiki uwanjani
12
Mizinga iwe ugani, na mbwembwe za askari,
Msafara mazikoni, pikipiki na magari,
Watu wale biriani, ya mchele wa pishori,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
13
Huenda hadi mwishoni, kabaki kuwa guberi,
Mumzike kihaini, mithili ya makafiri,
Mkumbuke na hisani, viumbe mtahayari,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
call/whatspp 0622845394 Morogoro
 
asante mkuu kwa shairi lako, ujumbe umefika na utafika
 
View attachment 381574

1
Hodi hodi kisimani, nina habari si nzuri,
Babu yetu Kigamboni, ameitwa na Qahari,
Jumbe si wa duniani, kaenda ile safari,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
2
Maisha yake huzuni, yajulikana dhahiri,
Katiwa kizuizini, ati si mtu mzuri,
Akatengwa Kigamboni, marufuku kusafiri,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
3
Alo yasema zamani, hadharani bila siri,
Kayatia kitabuni, mzee huyu jasiri,
MUUNGANO wa yakini, akafanya tafasiri,
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
4
Ikazuka tafarani, heri ikazaa shari,
Vyombo havielewani, vidau na manowari,
Kaskazi mkondoni, imechafuka bahari,
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
5
Katolewa mjengoni, urais ndo kwaheri,
Hakurudi na nyumbani, sasa miaka dahari,
Meli yake Magogoni, hakugusa Zanzibari,
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
6
"Kweli" itie shimoni, uichinje na buchari,
Ama itie motoni, jua tabaki ngangari,
Ipo siku tabaini, "kweli" ilivyo nawiri,
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
7
Turejee MAONI, ya katiba nashauri,
Mtaona naamini, Jumbe alivyoshamiri,
Miaka ni thelathini, mawazo bado ngunguri,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
8
Salamu toka kijani, tumepoteza hodari,
Kutoka serikalini, Jumbe kafa jasiri,
Tuwasute bila soni, zikome zao ghururi,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
9
Salamu za upinzani, Jumbe hakuwa hatari,
Haki alivyoamini, huletwa kwa kusubiri,
Ndio sababu jueni, isizuke halibari,
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
10
Wapinzani ahsanteni, na mtupe ikirari,
Siku gani hasa lini, mlikipanda kihori,
Mkenda kwake nyumbani, kumpa japo habari
Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.
11
Sasa niko tamatini, kufunga langu shairi,
Kuwauliza natamani, mjibu pasi dosari
Alofia gerezani, vipi watamstiri?
Tutawona dhahiri, wanafiki uwanjani
12
Mizinga iwe ugani, na mbwembwe za askari,
Msafara mazikoni, pikipiki na magari,
Watu wale biriani, ya mchele wa pishori,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
13
Huenda hadi mwishoni, kabaki kuwa guberi,
Mumzike kihaini, mithili ya makafiri,
Mkumbuke na hisani, viumbe mtahayari,
Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
call/whatspp 0622845394 Morogoro
Huyu atakuwa ni Profesa wa kiswahili si bure
 
Ningelikuwa ndo mm mwanae wangejitokeza hao serikali, Hiyo bendera ningeitoa kwa nguvu kweny geneza
 
Hata nyie mdaodiscuss ni kwasababu kashakufa mbona hamkufanya hivyo alipokua hai
 
Huu utenzi ni kama Nyimbo za Komba kwa Nyerere...
 
1)Hodi hodi kisimani, nina habari si nzuri,
Babu yetu Kigamboni, ameitwa na Qahari,Jumbe si wa duniani, kaenda ile safari,Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.

Maisha yake huzuni, yajulikana dhahiri,Katiwa kizuizini, ati si mtu mzuri,Akatengwa Kigamboni, marufuku kusafiri,Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.

Alo yasema zamani, hadharani bila siri,Kayatia kitabuni, mzee huyu jasiri,MUUNGANO wa yakini, akafanya tafasiri,Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.

Ikazuka tafarani, heri ikazaa shari,Vyombo havielewani, vidau na manowari,Kaskazi mkondoni, imechafuka bahari,Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.

Katolewa mjengoni, urais ndo kwaheri,Hakurudi na nyumbani, sasa miaka dahari,Meli yake Magogoni, hakugusa Zanzibari,Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.

"Kweli" itie shimoni, uichinje na buchari,Ama itie motoni, jua tabaki ngangari,Ipo siku tabaini, "kweli" ilivyo nawiri,Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.

Turejee MAONI, ya katiba nashauri,Mtaona naamini, Jumbe alivyoshamiri,Miaka ni thelathini, mawazo bado ngunguri,Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.

Salamu toka kijani, tumepoteza hodari,Kutoka serikalini, Jumbe kafa jasiri,Tuwasute bila soni, zikome zao ghururi,Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.

Salamu za upinzani, Jumbe hakuwa hatari,Haki alivyoamini, huletwa kwa kusubiri,Ndio sababu jueni, isizuke halibari,Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.

Wapinzani ahsanteni, na mtupe ikirari,Siku gani hasa lini, mlikipanda kihori,Mkenda kwake nyumbani, kumpa japo habari Tutawaona dhahiri, wanafiki hadharani.

Sasa niko tamatini, kufunga langu shairi,Kuuliza natamani, mjibu pasi dosari Alofia gerezani, vipi watamstiri? Tutawona dhahiri, wanafiki uwanjani

Mizinga iwe ugani, na mbwembwe za askari,Msafara mazikoni, pikipiki na magari,Watu wale biriani, ya mchele wa pishori,Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.

Huenda hadi mwishoni, kabaki kuwa guberi,Mumzike kihaini, mithili ya makafiri,Mkumbuke na hisani, viumbe mtahayari,Tutawaona dhahiri, wanafiki uwanjani.
 
Mzee umeweka namba ya simu ili Lumumba wakupigie simu ukaimbe utenzi huo msibani upewe buku 7, anyway ni ujasiriamali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom