Siyo kweli kuwa kila mtu ataamua, tunaokolewa si kwa mastahili yetu bali ni kwa neema tu.
Watu wanaishi hovyo ila dakika za mwisho kufani wanatubu ila wengine wanaishi vizuri mwishoni wanaharibu. Sisi binadamu tunashindwa kujua tumshangilie yupi kati ya hao wawili, na kwa vile hatutaki kumpangia Mwenyezi 'ampumzishe ANAPOSTAHILI' badala yake tunamuomba awape wote raha japo tunajua Mwenyezi atafanya kwa kadri apendavyo. Hoja yangu ni siyo busara kumtaka Mwenyezi ampumzishe mtu mahali fulani bali tumuombe ikiwezekana ampe mahali pema karibu naye yaani mwanga wa milele. Kwa kufanya hivyo tunakuwa tunajiombea huruma pia sisi wenyewe kwani hatustahili pia.Hiyo Neema si unaamua wewe mwenyewe ukiwa hai kwamba uikubali au ukatae? Neema imefunuliwa kwa watu wote, kila atakae anapokea. Huwezi kuniambia mtu alikua jambazi au mwizi na hakuwahi kupokea hiyo Neema akatengeneza maisha yake ukafikiri RIP itampeleka mbinguni. Matendo yake alipokua hai yataamua nafsi yake itaenda wapi.