Burian Alhaj Sheikh Ahmed Islam

Burian Alhaj Sheikh Ahmed Islam

Rubawa

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2015
Posts
2,055
Reaction score
3,263
*SHEIKH AHMED ISLAM NIMJUAE*

*Ramadhani K. Dau*

Ilikuwa siku ya Jumamosi tarehe 23 Disemba 2017, majira ya saa 5 usiku kwa saa za Malaysia nilipopata ujumbe mfupi wa sms kutoka kwa *Sheikh Issa Othman*, maarufu Mufti wa London, Imam wa Masjid Maamur ukiniarifu msiba wa mzee wetu Sheikh Ahmed Islam. Ujumbe wake ulikuwa mfupi sana: “Mzee wetu Ahmed Islam amefariki sasa hivi. Maiti inaletwa msikitini hivi sasa. Maziko kesho In Shaa Allah. Innallillahi Wainnaillahi Raajiuun”.

Mara tu baada ya kupata taarifa hiyo na baada ya kumtakia maghfira mzee wetu, nikajua kuwa kwa mara nyingine tena umeniangukia wajibu wa kuandika Taazia ya mtu ambaye namfahamu, namheshimu na alikuwa na ukaribu sana na mimi. Nimeshawahi kuandika huko nyuma kuwa kuandika Taazia ni jambo zito na gumu sana. Kila niandikapo hutamani sana Taazia hiyo iwe ndio ya mwisho. Lakini kwa mipango Yake Mwenyezi Mungu, najikuta nashindwa kukwepa wajibu huo. Hata hivyo, mara hii nilidhani ningeweza kuukwepa wajibu huo kwa kumuomba rafiki yangu na ndugu yangu mwanahistoria maarufu *Sheikh Mohamed Said* aandike Taazia hiyo nami nilikuwa tayari kumpa maelezo yoyote ambayo yangemsaidia katika uandishi wake. Pamoja ya kuwa alikubali kuifanya kazi hiyo, Mohamed alisisitiza kuwa lazima na mimi niandike. Kwa jinsi ya msisitizo aliouweka Sheikh Mohamed, nimejikuta kwa mara nyingine tena nalazimika kuandika Taazia hii huku nikiwa na moyo wa huzuni sana kwa kuondokewa na mzee wangu ambaye alikuwa mithili ya baba yangu mzazi.

Marehemu mzee Ahmed Islam ana mambo mengi na sura nyingi. Wapo wanaomfahamu kama ni miongoni mwa wazee maarufu na viongozi katika jamii ya Waislamu, wapo wanaomfahamu kama mtaalamu wa masuala ya Rasilimali Watu (Human Resources) na wapo wanaomfahamu mzee Ahmed Islam kama mwana michezo mahiri.
*Marehemu mzee Ahmed Ijhad Islam* alizaliwa Zanzibar tarehe 22 Disemba 1930 akiwa ni mtoto pekee wa Sheikh Ijhad Islam na bibi yetu Bi Maryam Mussa. Kwa bahati mbaya, mzee Ijhad Islam alifariki wakati mzee Ahmed akiwa mdogo na hivyo akalelewa na mama yake. Baada ya msiba huo, bibi yetu Bi Maryam aliolewa na kupata mtoto mmoja wa kike ambaye jina lake ni Zerah.
Baada ya kumaliza masomo yake ya msingi na Sekondari kwenye Government School (sasa Ben Bella) Zanzibar, mwaka 1957 marehemu mzee Ahmed Islam alikwenda Cornwall, Uingereza kuchukua masomo katika fani ya Mawasiliano yaani Telecommunications. Wakati huo alikuwa ameajiriwa na kampuni ya Cable and Wireless (C&W) ambako alikuwa Meneja Msaidizi (Assistant Manager). Baada ya kurudi masomoni, marehemu aliendelea na kazi yake na baada ya kampuni ya C&W kumezwa na Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki (East African Post and Telecommunication), mzee Islam akahamishiwa Dar es Salaam mwaka 1970.

Akiwa Dar es Salaam mzee Islam alifanyakazi katika Shirika hilo na baada ya mgawanyiko yakaundwa Mashirika mawili tofauti; Shirika la Posta (TPC) na Shirika la Simu (TTCL). Marehemu mzee Islam alihamishiwa TTCL hadi alipostaafu mwaka 1980 akiwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Rasilimali Watu yaani *Director of Manpower*. Baada ya kustaafu, marehemu alifanyakazi Ubalozi wa Ufaransa kwa mkataba wa miaka 3. Wakati wa uhai wake, mzee Islam amefanya mengi katika fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na uongozi wa dini, ujenzi wa nchi, uendelezaji wa michezo na utoaji nasaha kwa Taasisi na vijana mbalimbali katika masuala ya ndoa na kujiendeleza kwenye elimu ya juu.
*Kwa upande wa dini, marehemu ametoa mchango mkubwa sana*. Miongoni mwa matunda ya kazi yake ni usimamizi wa ujenzi wa Masjid Maamur iliyopo Upanga, Dar es Salaam. Kwa wanaokumbuka vizuri jiografia ya Upanga, pale palipojengwa Masjid Maamur hapakuwa na msikiti. Lakini kwa kushirikiana na wazee wenziwe marehemu mzee Islam aliweza kusimama kidete katika kusimamia ujenzi wa Masjid. Kana kwamba hiyo haitoshi, mwaka 2013, marehemu mzee Islam alichangia kwa kiasi kikubwa usimamizi wa ukarabati mkubwa wa msikiti huo kwa ufadhili mkubwa wa kampuni ya Oil Com.

Mbali na Masjid Maamur, marehemu mzee Islam pia alitoa mchango mkubwa sana katika ujenzi wa Masjid Ngazija hapa Dar es Salaam. Kwa bahati mbaya sana tokea ukoloni hadi leo, katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Central Business District), hakuna msikiti wowote mkubwa wala mdogo zaidi ya msikiti wa Ngazija. Lakini msikiti huo ambao ulijengwa wakati wa ukoloni ulikuwa ni mdogo sana kiasi cha kutokidhi mahitaji ya Waumini. Hivyo basi kwa kushirikiana na viongozi wengine kama vile marehemu *Sheikh Aboud Maalim, marehemu Profesa Haroub Othman Miraji, Sheikh Saidi Kassim, Habibu Nuru, AbdulHamid Mhoma* na wengineo, marehemu mzee Islam alishiriki kusimamia ujenzi wa msikiti mpya wa Ngazija ambao kwa sasa una ghorofa 3 na ndio msikiti pekee uliopo Dar es Salaam Central Business District. Pamoja na usimamizi wa ujenzi wa misikiti, mzee Islam ametunga vitabu mbali mbali vya dua na nyiradi na alikuwa mmoja wa wasimamizi wa uradi Masjid Ngazija kila Alhamisi.

Mchango wa marehemu mzee Islam katika kuwaendeleza vijana wa Kiislamu kielimu ni mkubwa bila kifani. Nina hakika si watu wengi wanaofahamu kuwa *mzee Ahmed Islam ndiye ambaye aliyefanikisha kupatikana kwa kiwanja ambacho kwa sasa imejengwa shule ya Sekondari ya AlHaramain jijini Dar es Salaam*. Naishauri BAKWATA ambayo ndio Wamiliki wa Shule ya AlHaramain wathamini mchango wa mzee Ahmed Islam kwa kulipa jina lake moja ya madarasa au kumbi za shule. Aidha mzee Islam alikuwa mstari wa mbele kwenye Taasisi ya Muslim Solidarity Trust Fund katika kusimamia nafasi za masomo za vijana wa Kiislamu wanaokwenda kusoma Uturuki kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Kiislam (Islamic Development Bank) iliyopo Jeddah, Saudi Arabia. Chini ya ufadhili huo, kwa karibu miaka 30 sasa Benki hiyo imekuwa ikifadhili vijana wa Kiislamu 15 kwenda kusoma masomo ya Uhandisi (Engineering) na Utabibu (Medicine) kwenye Vyuo Vikuu nchini Uturuki. Miongoni mwa watu walionufaika na mpango huu ni *Dr. Hussein Mwinyi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dr. AsanteRabi Kighoma Malima wa Chuo Kikuu cha Northeastern Marekani, Dr. Mashavu, daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama, Dr. Munawwara Kaguta daktari wa hospitali ya Aga Khan* na wengine wengi.

Moja ya mafanikio makubwa ya jitahada za marehemu mzee Islam ni uvumbuzi ambao ulifanywa mwezi Agosti 2014 na Dr. AsanteRabi Kighoma Malima ambaye alivumbua kifaa cha kuweza kubaini maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na saratani (cancer) yakiwa katika hatua za awali kabisa. Kutokana na uvumbuzi wa kifaa hicho ambacho amekiita Biolom, Dr. Malima alipewa tuzo na Gavana wa jimbo la Massachusetts, Bwana Deval Patrick. Haya ni matunda ya mzee wetu Ahmed Islam ambayo yameiletea sifa kubwa sana nchi yetu katika ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia.

Aidha mwaka 2002, mzee Islam *aliishawishi Taasisi ya Muslim Aid ya London kuja kujenga maabara 3 za kisasa katika shule ya Sekondari ya Twayyibat iliyopo Temeke Dar es Salaam*. Katika kipindi hicho hicho, kwa kupitia Muslim Aid, mzee Islam pia alifanikisha ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Sotele, Kisiju Mkoa wa Pwani. Harakati za marehemu mzee Islam kuwasaidia vijana katika kutafuta elimu hazikuanzia Dar es Salaam.

*Wakati akiwa Zanzibar, marehemu alikuwa akiwahimiza sana vijana kusoma na yeye binafsi alikuwa akijitolea kuwapa vijana mafunzo ya ziada (tuition) usiku kwa kutumia taa za kibatari*.

Marehemu mzee Islam alikuwa Mcha Mungu sana. Pamoja na kuwa na umri mkubwa wa miaka 87 na kuandamwa na maradhi ya miguu, kamwe hakuacha kuswali swala zote katika msikiti Maamur. Siku zote alikuwa wa kwanza kuingia msikitini na kuswali kwenye kiti msitari wa mbele. Mwaka 1997, *nilibahatika kusafiri kwenda Umra na marehemu mzee Islam* wakati Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) lilipofanya safari yake ya kwanza kwenda Jeddah, Saudi Arabia. Katika safari yetu walikuwepo *marehemu mzee Ahmed Rashad Ali, marehemu Siraju Juma Kaboyonga na mkewe marehemu Jaji Madina Muro, marehemu Prof. Haroub Othman, marehemu Balozi Selemani Hemedi, Dr. Idris Rashid, Jenerali Ulimwengu, mama Fatma Maghimbi, Mhe Hamad Rashid, mwanahistoria Sheikh Mohamed Saidi* na wengineo. Wengi walimshuhudia takriban kwa siku zote tulizokuwa safarini, marehemu mzee Islam alikuwa anaamka usiku kufanya ibada.

Mzee Islam alikuwa mtu wa watu na alikuwa mwepesi sana wa kusaidia watu wenye matatizo. Milango ya nyumba yake ilikuwa wazi saa zote ambapo watu wa rika zote walikuwa wanaenda kila siku kutaka misaada au ushauri. *Mzee Islam alikuwa jeshi la mtu mmoja na alikuwa zaidi ya Taasisi*. Hapa ntasimulia matukio mawili kati ya matukio mengi sana ambayo yanaonesha ukarimu na utayari wa marehmu katika kusaidia watu.

Siku moja mama mmoja kutoka mkoa wa Kilimanjaro alikwenda nyumbani kwa mzee Islam akiwa na watoto wa kike watatu ambao wote walikuwa yatima. Baada ya kueleza matatizo yake na ugumu wa maisha ya kulea wale mayatima, marehemu mzee Islam akamshauri wale watoto wabaki kwake na yeye atachukua jukumu la kuwalea na kuwasomesha. Yule mama akakubali rai ile. *Hivi niandikavyo Taazia hii*, mtoto mmoja amemaliza masomo ya Shahada ya kwanza katika Sheria (LLB) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kwa sasa anafanyakazi Tanga. Mwingine amemaliza Shahada ya Uzamili katika fani ya Uthamini vifaa vya ujenzi (Masters Degree in Quantity Survey) kwenye Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam. Na wa mwisho hivi sasa anachukua Stashahada (Diploma) ya Uhasibu.

Tukio lingine lilitokea mwaka 1991 wakati kijana mmoja alipokwenda nyumbani kwa mzee Ahmed Islam kumuomba msaada wa kwenda masomoni Ujerumani. Kama ilivyo kawaida yake, mzee Islam hakusita na alisimamia uchangishaji wa fedha kwa ajili ya safari masomo ya kijana huyo. *Leo hii, kijana huyo ni daktari bingwa nchini Ujerumani*. Mifano kama hii ipo mingi na nafasi haitoshi kuisimulia yote.

Kwa upande wa michezo, mzee Islam hakuwa nyuma. Wakati wa uhai wake, alikuwa mchezaji mzuri wa mpira wa miguu kiasi cha kuitwa mchawi wa mchezo huo. Alipokuwa Zanzibar alicheza timu ya Vikokotoni na timu ya Taifa ya Zanzibar. Akiwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar, mzee Islam alishiriki katika mashindano kadhaa ikiwemo mashindano maarufu ya kombe la Gossage akicheza namba 10. Mwaka 1952 timu ya Taifa ya Zanzibar ilifika fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika Nairobi Kenya na kushika nafasi ya pili baada ya kuzifunga timu za Tanganyika na Uganda. Pamoja wachezaji wengine, timu ya Zanzibar iliwakilishwa na marehemu *mzee Ahmed Islam, marehemu mz
 
Innalillah wa Inna Ilayh Raajiuun.
Naomba nitumie fursa hii kuipa pole familia ya marehemu kwa kuondokewa na kichwa cha familia,Allah awajaze subira katika kipindi hichi kigumu.Pia, nimpe pole Sheikh Dr Dau kwa kuondokewa na baba(hakuna jina jingine zaidi ya hili),serikali ya JMT na SMZ kwa kuondokewa na mshirika aliyesaidia kutetea na kuwapigania wananchi walio wengi kwenye juhudi za kuitafuta elimu.Jukumu hili lilikuwa ni sehemu ya marehemu kuisaidia serikali.Pia Watanzania wote kwa kuondokewa na baba yetu,mzee wetu na kipenzi chetu Mzee Islam.Kwangu mimi hili ni pengo kubwa na kunahitajika watu wenye moyo wa dhati kuweza kufanya angalau sehemu ya yale aliyoyasimamia.
Nikirudi kwa Dr Dau, nimekuwa mfuatiliaji wa Taanzia zako ambapo miezi michache nyuma, uliandika ukielezea wasifu wa marehemu mzee Kitwana Kondo ambaye hadhi yake kwako ni ile ya mzee Ahmadi Islam.Nakupongeza sana kwa kujenga utamaduni wa kuwa karibu na wazee hawa na wengine ambao ni hazina kubwa kwa taifa.Hongera sana kwa hilo.
Kwa imani hiyo hiyo,najua yapo mengi ambayo umekuwa ukiyapigania kwa manufaa ya jamii tangu ukiwa serikali na kwenye mashirika ya umma na wewe binafsi kama mzazi,mlezi au mzalendo uliyedhamiria kuwasaidia Watanzania.
Rai yangu kwako,nakuomba uendelee na moyo huo nikiamini itakuwa ni sehemu ya kuwaenzi wazee wetu MZEE KITWANA KONDO na MZEE AHMADI ISLAM ambao MwenyeziMungu amewapenda sana na kuamua kuwaita kwenye safari ya lazima kwa kila mwanadamu.
Allah akuongoze kuyasimamia haya.
 
RIP Sheikh Islam.
======
Sasa alisomesha kijana, na huyo kijana kakimbilia Germany! Anatusaidiaje sisi wahitaji wa huduma yake.
---
 
*SHEIKH AHMED ISLAM NIMJUAE*

*Ramadhani K. Dau*

Ilikuwa siku ya Jumamosi tarehe 23 Disemba 2017, majira ya saa 5 usiku kwa saa za Malaysia nilipopata ujumbe mfupi wa sms kutoka kwa *Sheikh Issa Othman*, maarufu Mufti wa London, Imam wa Masjid Maamur ukiniarifu msiba wa mzee wetu Sheikh Ahmed Islam. Ujumbe wake ulikuwa mfupi sana: “Mzee wetu Ahmed Islam amefariki sasa hivi. Maiti inaletwa msikitini hivi sasa. Maziko kesho In Shaa Allah. Innallillahi Wainnaillahi Raajiuun”.

Mara tu baada ya kupata taarifa hiyo na baada ya kumtakia magh**** mzee wetu, nikajua kuwa kwa mara nyingine tena umeniangukia wajibu wa kuandika Taazia ya mtu ambaye namfahamu, namheshimu na alikuwa na ukaribu sana na mimi. Nimeshawahi kuandika huko nyuma kuwa kuandika Taazia ni jambo zito na gumu sana. Kila niandikapo hutamani sana Taazia hiyo iwe ndio ya mwisho. Lakini kwa mipango Yake Mwenyezi Mungu, najikuta nashindwa kukwepa wajibu huo. Hata hivyo, mara hii nilidhani ningeweza kuukwepa wajibu huo kwa kumuomba rafiki yangu na ndugu yangu mwanahistoria maarufu *Sheikh Mohamed Said* aandike Taazia hiyo nami nilikuwa tayari kumpa maelezo yoyote ambayo yangemsaidia katika uandishi wake. Pamoja ya kuwa alikubali kuifanya kazi hiyo, Mohamed alisisitiza kuwa lazima na mimi niandike. Kwa jinsi ya msisitizo aliouweka Sheikh Mohamed, nimejikuta kwa mara nyingine tena nalazimika kuandika Taazia hii huku nikiwa na moyo wa huzuni sana kwa kuondokewa na mzee wangu ambaye alikuwa mithili ya baba yangu mzazi.

Marehemu mzee Ahmed Islam ana mambo mengi na sura nyingi. Wapo wanaomfahamu kama ni miongoni mwa wazee maarufu na viongozi katika jamii ya Waislamu, wapo wanaomfahamu kama mtaalamu wa masuala ya Rasilimali Watu (Human Resources) na wapo wanaomfahamu mzee Ahmed Islam kama mwana michezo mahiri.
*Marehemu mzee Ahmed Ijhad Islam* alizaliwa Zanzibar tarehe 22 Disemba 1930 akiwa ni mtoto pekee wa Sheikh Ijhad Islam na bibi yetu Bi Maryam Mussa. Kwa bahati mbaya, mzee Ijhad Islam alifariki wakati mzee Ahmed akiwa mdogo na hivyo akalelewa na mama yake. Baada ya msiba huo, bibi yetu Bi Maryam aliolewa na kupata mtoto mmoja wa kike ambaye jina lake ni Zerah.
Baada ya kumaliza masomo yake ya msingi na Sekondari kwenye Government School (sasa Ben Bella) Zanzibar, mwaka 1957 marehemu mzee Ahmed Islam alikwenda Cornwall, Uingereza kuchukua masomo katika fani ya Mawasiliano yaani Telecommunications. Wakati huo alikuwa ameajiriwa na kampuni ya Cable and Wireless (C&W) ambako alikuwa Meneja Msaidizi (Assistant Manager). Baada ya kurudi masomoni, marehemu aliendelea na kazi yake na baada ya kampuni ya C&W kumezwa na Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki (East African Post and Telecommunication), mzee Islam akahamishiwa Dar es Salaam mwaka 1970.

Akiwa Dar es Salaam mzee Islam alifanyakazi katika Shirika hilo na baada ya mgawanyiko yakaundwa Mashirika mawili tofauti; Shirika la Posta (TPC) na Shirika la Simu (TTCL). Marehemu mzee Islam alihamishiwa TTCL hadi alipostaafu mwaka 1980 akiwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Rasilimali Watu yaani *Director of Manpower*. Baada ya kustaafu, marehemu alifanyakazi Ubalozi wa Ufaransa kwa mkataba wa miaka 3. Wakati wa uhai wake, mzee Islam amefanya mengi katika fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na uongozi wa dini, ujenzi wa nchi, uendelezaji wa michezo na utoaji nasaha kwa Taasisi na vijana mbalimbali katika masuala ya ndoa na kujiendeleza kwenye elimu ya juu.
*Kwa upande wa dini, marehemu ametoa mchango mkubwa sana*. Miongoni mwa matunda ya kazi yake ni usimamizi wa ujenzi wa Masjid Maamur iliyopo Upanga, Dar es Salaam. Kwa wanaokumbuka vizuri jiografia ya Upanga, pale palipojengwa Masjid Maamur hapakuwa na msikiti. Lakini kwa kushirikiana na wazee wenziwe marehemu mzee Islam aliweza kusimama kidete katika kusimamia ujenzi wa Masjid. Kana kwamba hiyo haitoshi, mwaka 2013, marehemu mzee Islam alichangia kwa kiasi kikubwa usimamizi wa ukarabati mkubwa wa msikiti huo kwa ufadhili mkubwa wa kampuni ya Oil Com.

Mbali na Masjid Maamur, marehemu mzee Islam pia alitoa mchango mkubwa sana katika ujenzi wa Masjid Ngazija hapa Dar es Salaam. Kwa bahati mbaya sana tokea ukoloni hadi leo, katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Central Business District), hakuna msikiti wowote mkubwa wala mdogo zaidi ya msikiti wa Ngazija. Lakini msikiti huo ambao ulijengwa wakati wa ukoloni ulikuwa ni mdogo sana kiasi cha kutokidhi mahitaji ya Waumini. Hivyo basi kwa kushirikiana na viongozi wengine kama vile marehemu *Sheikh Aboud Maalim, marehemu Profesa Haroub Othman Miraji, Sheikh Saidi Kassim, Habibu Nuru, AbdulHamid Mhoma* na wengineo, marehemu mzee Islam alishiriki kusimamia ujenzi wa msikiti mpya wa Ngazija ambao kwa sasa una ghorofa 3 na ndio msikiti pekee uliopo Dar es Salaam Central Business District. Pamoja na usimamizi wa ujenzi wa misikiti, mzee Islam ametunga vitabu mbali mbali vya dua na nyiradi na alikuwa mmoja wa wasimamizi wa uradi Masjid Ngazija kila Alhamisi.

Mchango wa marehemu mzee Islam katika kuwaendeleza vijana wa Kiislamu kielimu ni mkubwa bila kifani. Nina hakika si watu wengi wanaofahamu kuwa *mzee Ahmed Islam ndiye ambaye aliyefanikisha kupatikana kwa kiwanja ambacho kwa sasa imejengwa shule ya Sekondari ya AlHaramain jijini Dar es Salaam*. Naishauri BAKWATA ambayo ndio Wamiliki wa Shule ya AlHaramain wathamini mchango wa mzee Ahmed Islam kwa kulipa jina lake moja ya madarasa au kumbi za shule. Aidha mzee Islam alikuwa mstari wa mbele kwenye Taasisi ya Muslim Solidarity Trust Fund katika kusimamia nafasi za masomo za vijana wa Kiislamu wanaokwenda kusoma Uturuki kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Kiislam (Islamic Development Bank) iliyopo Jeddah, Saudi Arabia. Chini ya ufadhili huo, kwa karibu miaka 30 sasa Benki hiyo imekuwa ikifadhili vijana wa Kiislamu 15 kwenda kusoma masomo ya Uhandisi (Engineering) na Utabibu (Medicine) kwenye Vyuo Vikuu nchini Uturuki. Miongoni mwa watu walionufaika na mpango huu ni *Dr. Hussein Mwinyi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dr. AsanteRabi Kighoma Malima wa Chuo Kikuu cha Northeastern Marekani, Dr. Mashavu, daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama, Dr. Munawwara Kaguta daktari wa hospitali ya Aga Khan* na wengine wengi.

Moja ya mafanikio makubwa ya jitahada za marehemu mzee Islam ni uvumbuzi ambao ulifanywa mwezi Agosti 2014 na Dr. AsanteRabi Kighoma Malima ambaye alivumbua kifaa cha kuweza kubaini maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na saratani (cancer) yakiwa katika hatua za awali kabisa. Kutokana na uvumbuzi wa kifaa hicho ambacho amekiita Biolom, Dr. Malima alipewa tuzo na Gavana wa jimbo la Massachusetts, Bwana Deval Patrick. Haya ni matunda ya mzee wetu Ahmed Islam ambayo yameiletea sifa kubwa sana nchi yetu katika ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia.

Aidha mwaka 2002, mzee Islam *aliishawishi Taasisi ya Muslim Aid ya London kuja kujenga maabara 3 za kisasa katika shule ya Sekondari ya Twayyibat iliyopo Temeke Dar es Salaam*. Katika kipindi hicho hicho, kwa kupitia Muslim Aid, mzee Islam pia alifanikisha ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Sotele, Kisiju Mkoa wa Pwani. Harakati za marehemu mzee Islam kuwasaidia vijana katika kutafuta elimu hazikuanzia Dar es Salaam.

*Wakati akiwa Zanzibar, marehemu alikuwa akiwahimiza sana vijana kusoma na yeye binafsi alikuwa akijitolea kuwapa vijana mafunzo ya ziada (tuition) usiku kwa kutumia taa za kibatari*.

Marehemu mzee Islam alikuwa Mcha Mungu sana. Pamoja na kuwa na umri mkubwa wa miaka 87 na kuandamwa na maradhi ya miguu, kamwe hakuacha kuswali swala zote katika msikiti Maamur. Siku zote alikuwa wa kwanza kuingia msikitini na kuswali kwenye kiti msitari wa mbele. Mwaka 1997, *nilibahatika kusafiri kwenda Umra na marehemu mzee Islam* wakati Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) lilipofanya safari yake ya kwanza kwenda Jeddah, Saudi Arabia. Katika safari yetu walikuwepo *marehemu mzee Ahmed Rashad Ali, marehemu Siraju Juma Kaboyonga na mkewe marehemu Jaji Madina Muro, marehemu Prof. Haroub Othman, marehemu Balozi Selemani Hemedi, Dr. Idris Rashid, Jenerali Ulimwengu, mama Fatma Maghimbi, Mhe Hamad Rashid, mwanahistoria Sheikh Mohamed Saidi* na wengineo. Wengi walimshuhudia takriban kwa siku zote tulizokuwa safarini, marehemu mzee Islam alikuwa anaamka usiku kufanya ibada.

Mzee Islam alikuwa mtu wa watu na alikuwa mwepesi sana wa kusaidia watu wenye matatizo. Milango ya nyumba yake ilikuwa wazi saa zote ambapo watu wa rika zote walikuwa wanaenda kila siku kutaka misaada au ushauri. *Mzee Islam alikuwa jeshi la mtu mmoja na alikuwa zaidi ya Taasisi*. Hapa ntasimulia matukio mawili kati ya matukio mengi sana ambayo yanaonesha ukarimu na utayari wa marehmu katika kusaidia watu.

Siku moja mama mmoja kutoka mkoa wa Kilimanjaro alikwenda nyumbani kwa mzee Islam akiwa na watoto wa kike watatu ambao wote walikuwa yatima. Baada ya kueleza matatizo yake na ugumu wa maisha ya kulea wale mayatima, marehemu mzee Islam akamshauri wale watoto wabaki kwake na yeye atachukua jukumu la kuwalea na kuwasomesha. Yule mama akakubali rai ile. *Hivi niandikavyo Taazia hii*, mtoto mmoja amemaliza masomo ya Shahada ya kwanza katika Sheria (LLB) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kwa sasa anafanyakazi Tanga. Mwingine amemaliza Shahada ya Uzamili katika fani ya Uthamini vifaa vya ujenzi (Masters Degree in Quantity Survey) kwenye Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam. Na wa mwisho hivi sasa anachukua Stashahada (Diploma) ya Uhasibu.

Tukio lingine lilitokea mwaka 1991 wakati kijana mmoja alipokwenda nyumbani kwa mzee Ahmed Islam kumuomba msaada wa kwenda masomoni Ujerumani. Kama ilivyo kawaida yake, mzee Islam hakusita na alisimamia uchangishaji wa fedha kwa ajili ya safari masomo ya kijana huyo. *Leo hii, kijana huyo ni daktari bingwa nchini Ujerumani*. Mifano kama hii ipo mingi na nafasi haitoshi kuisimulia yote.

Kwa upande wa michezo, mzee Islam hakuwa nyuma. Wakati wa uhai wake, alikuwa mchezaji mzuri wa mpira wa miguu kiasi cha kuitwa mchawi wa mchezo huo. Alipokuwa Zanzibar alicheza timu ya Vikokotoni na timu ya Taifa ya Zanzibar. Akiwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar, mzee Islam alishiriki katika mashindano kadhaa ikiwemo mashindano maarufu ya kombe la Gossage akicheza namba 10. Mwaka 1952 timu ya Taifa ya Zanzibar ilifika fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika Nairobi Kenya na kushika nafasi ya pili baada ya kuzifunga timu za Tanganyika na Uganda. Pamoja wachezaji wengine, timu ya Zanzibar iliwakilishwa na marehemu *mzee Ahmed Islam, marehemu mz
Innah lillah wainnah ilayh rajioon Allah afanye kaburi liwe ni moja ya bustani za peponi in shaa Allah
 
Maisha mazuri Na yenye mwisho mwema.
Allah akupe Nuru kaburini Na Akhera pia.
Akukubali In shaa Allah.
 
SHEIKH AHMED ISLAM (1930 - 2017) NA MOHAMED SAID
 
Back
Top Bottom