Kimsingi bunge ni muhimili unaojitegema kama ilivyo mahakama na serikali. Mihimili hii yote ni lazima iwe na uhuru wake na kutoingiliwa na muhimili au mihimili mingine.
Kwa kujua, kudhamilia na kwa makusudi serikali uwa inaingilia mihimili mingine (mahakama na bunge) katika maamuzi wao. Kwa mfano kwanini mwanasheria mkuu wa serikali, mawaziri, baadhi ya wakuu wa mikoa ambao kimsingi ni watendaji wa serikali waingie bungeni kutoa maamuzi. Kwa nini Mh. Spika awe ni mjumbe wa halmashauri ya chama tawala .... atatenda haki???? Kama haitoshi kwa nini Mh. rais ateue jaji mkuu na majaji wengine wakati ni muhimili mwingine tofauti????. Nadhani katiba mpya (ikiendeshwa vizuri) itakuwa ni jibu tosha kwa maswali haya na mengine ya wengine.