YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,992
Bunge letu linatakiwa liwe na msemaji au ofisa habari wa bunge ambaye kazi yake itakuwa kukusanya taarifa zote za kilichoendelea bungeni kila siku na kuwapa waandishi wa habari na vyombo vya habari.
Sasa hivi Bunge limekuwa kama gulio la waandishi na vyombo vya habari ambamo kila chombo na mwandishi wa habari ni ofisa habari wa bunge.
Hakuna haja ya vyombo vya habari kujazana kama wako mnadani ndani ya bunge.Lile ni eneo la kazi jamani.Tuache wabunge wafanye kazi wakimaliza kufunga siku ofisa habari atoe press release na video vya mambo muhimu yaliyofanyika ambayo ni muhimu wananchi wayajue na yale yanayowasaidia.
Kujazana waandishi makanjanja bungeni kunatupotezea muda.Mbunge akikohoa wanaandika mbunge akohoa,akizomea mbunge azomea au azomewa, ujinga mtupu.
Kuwepo mfumo rasmi wa kutoa habari wa kueleweka na hili lawezekana tu kwa kuwa na ofisa habari wa bunge ambaye ni official.Vyombo vya habari visiwemo kabisa ndani ya bunge likiwa kazini bungeni visubiri press release toka kwa ofisa habari.
Halafu wabunge waelewe wananchi hatukuwatuma kuuza sura kwenye TV tunataka maendeleo kwenye majimbo.Yaani wabunge wanapigania sura zao kuonekana kwenye TV hatutaki kuona sura zenu wala sauti zenu wabunge kwenye TV tunataka maendeleo majimboni