Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
Hatua za bunge la Tanzania dhidi mkuu wa mkoa wa DSM zinatuthibitishia UGUMU wa VITA ya MADAWA ya KULEVYA ulivyo si Tanzania tu bali dunia nzima.
Jiulize kwanini nchi kama Marekani yenye kila aina ya tekinololijia ya usalama na vifaa vya usalama lakini MADAWA yapo na yanauzwa kama njugu.
Sababu nyepesi tu, wale waliopewa mamlaka ya maamuzi na kuongoza nchi kwa namna moja au nyingine ni wanufaika wa mojakwamoja au sio wa mojakwamoja WA BIASHARA ya madawa ya kulevya.
Wanufaika kama hawa hawatakubali biashara hii ikomeshwe wakati pesa za kampeni za kuingia ikulu na bungeni wanapata katika biashara ya unga.
Kwa mtu mwenye akili ataelewa tu, hawa wabunge wa upinzani na wa CCM ni kama chui na paka na kuna mambo ya msingi kabisa tumeona mara nyingi hawafikiani na hawapatani kiasi wabunge wa upinzani wasuse na watoke nje.
Lakini hili la MAKONDA kuwajibishwa, wameungana, wenye akili lazima wajiulize huu urafiki ni wa kweli uliochipua sasa au ni ufarafiki wa kulinda maslahi yao?
Bunge kwa kauli moja limemshughulikia Makonda??? Kwanini hii kauli moja haipatikani kwa IPTL??? kwanini hii kauli moja haipakani MEREMETA?? hii kauli moja kwanini haipo kwenye kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na bima ya afya? Hii kauli moja kwanini haipo katika kuhakikisha kila mzee anapewa fedha za kujikimu kila mwezi? Hii kauli moja kwanini haipo juu uandikwaji wa katiba mpya?
Lakini tumeona kauli moja dhidi Makonda anayepambana na WAUZAJI WA UNGA, hili ni tangazo la vita dhidi yetu watanzania na si kwa Makonda.
Ingekuwa nchi za wenzetu, nchi zilizo endelea, jana ukumbi wa bunge ungezingiriwa na wananchi, ambao wangewazuia wabunge wao kutoka nje ya ukumbi wa bunge hadi wabadili maamuzi yao yaliyoongozwa na mslahi ya wauza unga badala ya maslahi ya umma.
Jambo la ajabu ukitaka kujua mtandao wa madawa ya kulevya na wanufaika wao, jaribu kuorodhesha watu ambao sasa unadhani wanamchukia Makonda.
Mimi naanza.
Kanisa......Gwajima
Yanga........Baadhi ya Viongozi
Wasanii.......na mashabiki/wapambe zao
Wafanyabiashara
CCM....wabunge
CHADEMA...wabunge
CUF................wabunge
ACT................wabunge
Yanga............%kubwa ya mashabiki
CHADEMA.....%kubwa ya wanachama
CUF................%kubwa ya wanachama
ACT.................%kubwa ya wanachama
........
Wengine jaza wewe.
Hawa wote huenda ni wanufaika wa madawa ya kulevya aidha mojakwamoja au sio mojakwamoja na huenda wanatumia kivuli cha bunge kuhalalisha chuki na vita yao dhidi ya Makonda.
Kwa silisili hii, ningekuwa na mamlaka ningeamuru ufanyike uchunguzi wa kifo cha Amina Chifupa, sanjari na kumuongezea Makonda ulinzi maradufu kutoka kwa askari ambao ni wazalendo wa nchi hii, ila khofu isingeisha sababu mtandao madawa mkubwa sana na upo katika kila sehemu, na hao askaru kwa vyovyote vile wasingetoka mbinguni.
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whats app 0622845394 Morogoro.