Bunge lamlilia Dkt. Reginald Mengi

Bunge lamlilia Dkt. Reginald Mengi

RUKIA MBONDE

Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
64
Reaction score
50
1086998


Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa niaba ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ameungana na Watanzania kuomboleza kifo cha Dkt. Reginald Mengi na kueleza mchango wake mkubwa kwa taifa.

Spika Ndugai ametumia dakika mbili kuoeleza mchango wa Dkt. Mengi katika Taifa na namna wakavyomkumbuka.

"Katika kuomboleza kifo sisi Bunge tunaungana na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, familia ya marehemu na Watanzania wote tukimshukuru Mwenyenzi Mungu na kumshukuru Mhe. Mengi kwa mchango wake mkubwa usiopimika kwetu Watanzania," amesema Spika.

Dkt. Reginald Mengi ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, alifariki usiku wa kuamkia jana akiwa Dubai.
 
Bunge dhaifu, hii inatokea tanzania tu bunge kumlilia mtu mmoja tu wakati kuna wanajeshi wetu wanakufa DRC hawajawahi hata kutoa pole
 
Hapo NDUGAI na yule NAIBU wake wajifunze kuwa na wao watakufa kama alivyokufa mzee wetu Mengi! Nakumbuka Siku tulia anazuia mapendekezo ya wabunge wengi kujadili mishahara!!!!???? Halafu nikasikia kuwa yeye in mlokole aiseee nilishangaa. Tulia kama utaona Uzi huu nashauri ujitakase na utubu kwa mola wako tofauti na hapo.......! mi sina zaidi cha kusema.
 
Back
Top Bottom