Bunge Lachafua Waandishi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
CHAMA cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (OJADACT), kimetoa mtako la kupinga vikali kitendo cha waandishi wa habari kuzuiwa kuingia bungeni kufanya kazi za ukusanyaji taarifa,

Ojadact imeeleza kuwa, hatua ya kuwazuia waandishi wa habari kuingia bungeni ili kutimiza majukumu yao ya kitaaluma bila sababu za msingi ni uonevu mkubwa pia ukiukwaji wa haki za msingi.

Edwin Soko, mwenyekiti wa chama hicho amesema, wanasikitishwa na kitendo kilicho tokea jana mjini Dodoma kwenye vikao vya Bunge la Bajeti kwa waandishi kukatazwa kuingia bungeni, ni mwendelezo wa ajenda ya siri ya serikali dhidi ya kuminya Uhuru wa kupata taarifa kwa wananchi na kuogopa serikali kukosolewa.

Amesema kitendo hicho si tu kinaviumiza vyombo vya habari lakini pia vinaumiza jamii na kuinyima haki ya kujua mambo mbalimbali yanayohusu nchi yao wakati yakijadiliwa na wawakilishi wao.

Aidha amezitaja sababu ambazo zinapelekea waandishi kuzuiwa kuingia Bungeni ni suala la mpango wa Bunge kuwa dawati la habari za bunge pekee na wengine kuchukua huko, ambalo halikukubaliwa na wabunge kabla ya utekelezaji wa azimio hilo.

Pamoja na suala la utaratibu wa mabunge ya jumuiya ya madola kurusha matangazo ya bunge kupitia chaneli ya bunge sio sababu ya msingi kwani mabunge hayo yana utaratibu mwingine wenye haki na usawa wa uendeshaji wa shughuli za bunge tofauti na Tanzania.

Ikumbukwe kuwa serikali lianza kwa kutoa tamkola la runinga ya serikali TBC,kutorusha vikao vya Bunge wakati wote kwa madai kutokuwa na fedha,kwa bahati nzuri taasisi ya wakfu wa tasnia ya habari Tanzania (TMF)ikatoa tamko la kutaka kutoa fedha za kufanikisha kurushwa kwa matangazo hayo kama awali lakini serikali imekaa kimya hadi sasa.

Soko ameitaka serikali ya awamu ya tano kuheshimu waandishi wa habari na kuwaruhusu kuendelea na majukumu yao ya kuripoti vikao vya bunge kama zamani bila zuio lolote na kusisitiza kuwa serikali isiogope kukosolewa kwani ni tika ya kujipima katika hufanyaji kazi wake.
 
Hii nchi kwa kweli, huyu kila siku anadai tumuombee kwa lipi hasa? Bunge hutaki tuonyeshwe ili.................? Sokoine wa enzi hizi anatisha.
 
Hakuna lolote ni Wimbo ule ule wana danganya watu wa Vijijini c town
 
Hivi kama issue ni muda wa Kazi, kwa nini CCM/SERIKALI isiviagize vyombo vyote vya habari kuzima mitambo yao na kuiwasha baada ya muda wa Kazi kuisha lakini pia serikali ipige marufuku Kazi zote zinavyofanywa usiku kama vile Kazi za hospital, migodini,security service na nk.
Au kama hilo la kisitisha NIGHT SHIFTS zote litashindikana basi ufanyike utaratibu wa kubadili ratiba ya vikao vya BUNGE badala ya kukaa mchana basi Bunge likae Usiku ili wananchi waweze kufuatilia kile kinachofanywa na wawakilishi wao katika MUHIMILI huo.
 
Back
Top Bottom