Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha bajeti ya shilingi Trilioni 29.5 ya mwaka wa fedha 2016/17 ambayo iliwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango June 08, 2016.
Bajeti hiyo ilipigiwa kura na wabunge waliokuwepo bungeni, ambapo jumla ya wabunge 251 walipiga kura za ndio za kuipitisha bajeti hiyo kati ya wabunge 252 waliokuwepo ukumbini wakati kura hizo zikipigwa.
Katika kupiga kura Hakukuwa na kura yoyote ya hapana au kutokuamua kati ya wabunge waliopiga kura. Jumla ya wabunge 137 hawakuwepo wakati kura zinapigwa.“Naipongeza Serikali kwa kutoa hoja ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17 na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, namtakia Waziri wa Fedha kila la heri katika hatua zinazofuata katika utekelezaji wa bajezi hii,” alisema Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
Aidha bunge hilo, lilipitisha muswada wa sheria za Serikali kuidhinisha Trilioni 29.5 kwa matumizi ya Serikali kutoka mfuko wa hazina kwa mwaka unaoishia June 30, 2016. Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango amewataka watanzania kulipa kodi na wale wote wanaotakiwa kusimamia ukusanyaji wa kufanya kazi hiyo kwa ukamilifu ili fedha zilizopitishwa katika bajeti ya mwaka 2016/17.
Sheria hiyo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inasubiri kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo utekelezaji wake utaanza Julai 01, 2017.
Chanzo: MichuziJr