Bunge la Seneti kuchapisha ushahidi unaomshutumu Rais Trump

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
trump.jpg

Kamati ya Bunge la Seneti la masuala ya usalama nchini Marekani imechapisha ushahidi utakaotolewa na mkurugenzi aliyetimuliwa kazi FBI ambaye amesema Rais Trump alimtaka mkurugenzi huyo kuacha kumchunguza mshauri wa zamani wa masuala ya usalama.

James Comey alitoa uchambuzi wa ushaidi wa mazungumzo kati yake na rais Trump aliyofanya naye mara tano wakati Trump alipokuwa akirudia kutaka amsikilize na kumheshimu wakati ambapo Comey anasema alikuwa akifanya kazi zake bila kuegemea upande wowote.

Wakili wa Trump amesema rais Trump anahisi kuna ukweli kwa uthibitisho kuwa yeye mwenyewe binafsi hakuwa akichunguzwa kwa timu yake ya kampeni zake kuhusishwa na Urusi.

Maafisa wawili wanaohusika na usalama,Mike Rogers na Dan Coats wamewaambia maseneta kuwa hawakuwahi kulazimishwa kufanya jambo lolote ambalo liko kinyume na sheria.

Lakini wakati wa kikao cha kamati ya Seneti siku ya Alhamisi, Bwana Comey ataeleza kwa kina jinsi Bwana Trump alisababisha ashikwe na wasi wasi kabla ua kufutwa mkurugenzi wa FBI tarehe 9 mwezi Mei.

Hii ni moja ya majopo pamoja na idara ya sheria, kuchunguza ripoti za mashirika ya ujasusi ya Marekani kuwa wadukuzi wa Urusi waliingilia kati uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba.

Pia kuna uchunguzi kuhusu ikiwa kundi la kampeni ya Trump lilishirikiana na wadukuzi wa Urusi madai ambayo Urusi inayakanusha.

Chanzo: BBC Swahili
 
Watahangaika weee ila hawawezi mtoa Trump
nimeisoma ile sijaona la maana
 
Kuna wakati nahisi Putin anamblackmail Trump
Endelea kuhisi tu.Na siku ikisikia hisia zako ni za kweli,basi kesho yake hutomuona Trump makdarakani,Impeachment itapigwa fasta tuu,Wamarekani huw hawana mchezo kwenye ishue za usalama wa nchi yao.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hakuna president anaye pitia kipindi kigumu kama trump,kuna usemi unasema malipo ni hapahapa duniani alimchukia sana obama sasa mambo yamembadilikia kuna uwezekano mkubwa wakamng'oa madarakani
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom