MGOGO27
JF-Expert Member
- Jan 5, 2016
- 459
- 217
Kama kichwa cha habari hapo juu, wewe unadhani kuna tija yoyote au waache wakajadiliane na kuja na utendaji kwani mimi nadhani ku edit na kurusha saa 5 usiku haina maana yoyote???
Wewe unaonaje, karibuni sana.
==============
Michango Mingine;
Wewe unaonaje, karibuni sana.
==============
Michango Mingine;
Zifuatazo ni athari za Bunge kutokuonyeshwa live:
1.Wabunge kukosa hamasa ya kazi
2.Wabunge wavivu kuzidi kuwa wavivu zaidi
4.Wabunge wanaosinzia Bungeni kuongezeka
5.Wananchi kukosa hamasa ya kufuatila habari za Bunge
6.Kuna uwezekano wa mapungufu ya wabunge wa chama fulani kufichwa ili hali yale ya wa wabunge wa upande wa pili kuonyeshwa katika vipindi vya marudio(recorded) vya Bunge
7.Upo uwezekano wa baadhi ya wabunge kupewa airtime kubwa kuliko wengine na wengine kupewa muda mchache na wengine kukosa kabisa nafasi hiyo.
8.Vijana wanaochipukia katika siasa kukosa fursa ya kuona wabunge /wanasiasa ambao wanaweza kuwa ni Role model wao katika siasa.
9.Mahudhurio ya wabunge yanaweza kuwa mabovu kuliko ilivyowahi kuwa kwa siku za nyuma
10.Miswaada mibovu na isiyo na maslahi kwa nchi na wananchi inaweza kupitishwa kirahisi zaidi
11.Wananchi watakosa fursa ya kupima/kuona uwezo na ubora wa wabunge wao katika kuwatumika hasa wale wabunge wageni.
12.Wabunge wa viti maalumu wanaokusudia kugombea katika chaguzi zijazo kukosa fursa ya kuonyesha uwezo wao ndani ya Bunge.
13.Uwezekano wa kuongezeka kwa lugha zisizo na staha ndani ya Bunge.
14.Kwakuwa watanzania wengi ni wavivu wa kusoma,baadhi ya mambo yatakayojiri Bungeni watanzania wengi hawatayajua yakiwemo yale yanayohusu majimbo yao.
15.Kutotatuliwa kwa baadhi ya kero majimboni wananchi watashindwa kujua kuwa ni kutokana na mbunge wao kutotimiza wajibu wake ndani ya Bungeni au ni kutokana na serikali kutosikiliza kilio cha mbunge wao Bungeni.
16.Kupungua kwa idadi ya vijana watakaohamasika kujiunga na siasa na hivyo kuna baadhi ya vipaji vya wanasiasa wanaochipukia tutavipoteza.
Hizo ni baadhi tu ya athari za Bunge kutokurushwa live.Unaweza pia kuongeza zingine.