Hayo yalielezwa jana na madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bunda katika kikao cha robo ya tatu cha baraza la madiwani.
Baadhi ya madiwani walisema katika kata zao, baadhi ya wanaume wamezitelekeza familia zao kwa sababu mbalimbali, ikiwamo ya upungufu wa chakula.
Diwani wa Balili, Thomasi Tamuka, alisema upungufu wa chakula katika kata zao imetokana na ukame na tembo wanaotoka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushambulia mazao ya wakulima na kwenye maghala ya kuhifadhia chakula majumbani mwao.
Madiwani walisema tatizo jingine ambalo wanakabiliana nalo kwa sasa ni mahindi waliyokuwa Wanaume wakimbia familia kwa njaa “Kuna baadhi ya wanaume wamezitelekeza familia zao kwa sababu ya njaa, sasa sisi tunashangaa sana kuona chakula kilicholetwa na serikali kinakwenda katika halmashauri ya wilaya tu na kuiacha halmashauri yetu ya mji,”alisema Tamuka.
Chanzo: Nipashe