..u r 100% correct.
..Marekani na Uingereza wanaweza kuwa wanakupiga vita lakini bado makampuni yao yakaendelea kuwekeza nchini kwako.
..kwa mfano, wakati vita vya Angola[mpla vs unita], serikali ya Marekani ilikuwa inasaidia unita[waasi], wakati exxon mobil wanachimba mafuta cabinda na uwekezaji wao ndiyo una-finance war chest ya mpla[serikali]. wakati huo huo majeshi ya cuba ndiyo yalikuwa yanalinda visima vya mafuta vya serikali ya angola.
..jambo lingine nadhani tunafanya makosa kwa kujikita kuona ni nchi gani zitatuwekea vikwazo, na athari za vikwazo hivyo. hali hiyo ni sawa na kuangalia tulipoanguka badala ya wapi tumejikwaa.
..tukubali kwamba tumeboronga ktk uchaguzi marudio wa znz. tunachotakiwa kufanya ni kuchukua hatua ambazo zitashawishi nchi wahisani kuona kwamba tunatafuta suluhisho la kudumu la mgogoro wa znz.
JokaKuu nadhani unafahamu mzizi wa tatizo la Zanzibar.
Tatizo la Zanzibar siyo itikadi za kisiasa bali ni ubaguzi lakini vile vile kumbuka hatujaboronga katika uchaguzi huu tu, tumeanza kuboronga siku ambayo tulituma wanajeshi zaidi ya 300 ili kutoa ulinzi kwa Amani Karume na hapo hapo tukaamua kuungana na katika maisha yote ya muungano kabla ya vyama vingi, tumeshuhudia matatizo mengi.
Wakati Tanzania Bara wanaongelea Marais watano, Zanzibar imekuwa na Marais saba.
Nchi za Western zinachofanya ni kutumia matatizo haya kama opportunity katika ku-set agenda zao za kiuchumi ili ziwanufaishe.
Kuna mahojiano yalifanywa na Maalim Seif ambayo ukiyachunguza utaona hali halisi ya matatizo ya Zanzibar. Maalim Seif alinukuliwa akisema,“Kabla Kikwete (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) hajaondoka madarakani, aliniambia kuwa Maalim CCM wanakuogopa, wanajua ukishinda utaweza kuvunja Muungano, lakini nilimwambia, CCM ndio wenye jeshi, wenyewe ndio wenye dola mimi nitavunjaje Muungano’’.
Kama haya maelezo ni kweli basi yanatoa picha kuwa Rais wa Tanzania/Mwenyekiti wa CCM Taifa hana nguvu lilopokuja suala la Zanzibar. Kuna nguvu zaidi ya Rais ambazo zinafanya maamuzi kuhusu hatima ya Zanzibar.
Suala la kujiuliza, kina nani zaidi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania ndani ya CCM ambao wanaogopa Maalim Seif kuwa Rais wa Zanzibar kwa sababu atavunja Muungano? Au chenye nguvu ni ''Kitengo'' kilichokuwa kinasemwa na Mzee Kingunge ambacho tunaambiwa ndicho kinachofanya hata maamuzi kuhusu mgombea Urais wa CCM.
Kumbuka kwa kiwango kikubwa CCM bado ni chama dola kama ilivyokuwa kwenye siasa za chama kimoja!