BRELA huduma kwa wateja pokeeni simu za wateja

BRELA huduma kwa wateja pokeeni simu za wateja

cheguevara

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
1,348
Reaction score
653
Habarini wadau,

BRELA ni moja ya taasisi muhimu kwenye sekta ya uchumi wa nchi hii lakini imeoza kabisa kwa utoaji huduma hasa kwenye mawasiliano.

Huduma kwa wateja hawapokei simu kabisaaa tangu jana pasipo sababu za msingi na baadhi ya huduma ka kufungua makampuni hawashughulikii kabisa maombi mapya kwa wiki mbili sasa.

Kinachofanyika wanawapatia vishoka tracking no,mawasiliano/simu na majina ya makampuni yanatosajiliwa na vishoka kupiga simu kuomba hela ili wakimbize maombi yako wakijidai wako BRELA.

Pia wamejariri namba za wateja ambao wamegoma kushirikiana na vishoka wao na kutozipokea kabisa zinapopiga kuomba msaada.

Uongozi uliangalie hili na ikiwezekana wapitie simu za brela waone jinsi tunavyopiga simu hazipokelewi na kuwahoji waliokuwa mapokezi jana na leo kwanini simu hizo za wateja hazikupokelewa.

Pia wapitie maombi yote mapya yaliyowasilishwa ndani ya wiki hizi mbili na kutofanyiwa kazi wahoji kwanini hayajanyiwa kazi.

Mwisho tunashauri wahusika wabadilishwe kwani ni mzigo kwa taifa na wanakula mshahara wa bure.
 
Hili bado ni tatizo kubwa mpaka leo October 2023, ni wiki nzima imekwisha bila majibu yao na simu hazipokelewi. Usajili wa majina ya biashara unamaliza wiki na malipo yashafanyika sasa sijui kamouni usajili utachukua muda gani. Afrika tunasafari ndefu sana, pamoja na kupewa mshahara bado mtu anataka apewe hongo kufanya majukumu yake.
 
Back
Top Bottom