Bora nisingeisikia

Bora nisingeisikia

KICHUMVI

Senior Member
Joined
Aug 12, 2012
Posts
113
Reaction score
14
Kwa ufupi! siku moja nilipokuwa nimekwenda kwa rafiki yangu nilikutana na dada yake akanitambulisha Baada ya kama mwezi nikamuomba rafiki yangu namba ya huyo dada yake alinipa, nikampigia nikajitambulisha akanikumbuka baada ya hapo tukawa tunachat, huyo dada ni mfanyakazi ila kwasasa yupo kimasomo morogoro ktk chuo kikuu fulan hivi,basi ukaribu wetu uliongezeka kila siku tunawasiliana kwa sms na kwa kupigiana kwa simu kwa muda mrefu mno,baada ya miezi kama 8 hivi nikaamua kufunguka na kuomba mahusuino nae ya kimapenzi na baadae tuwe mume na mke kiukwel hakukubal kiraisi kwan ameshawahi kutendwa hivyo hakupenda kutendwa tena na hana iman na mwanaume yoyote tena nilijitahidi kuwa wazi kwake na hatimae alikubali na alionesha ni mwanamke mwenye msimamo kweli na asiependa ujinga ktk mahusiano ndio maana sikuwa na papara kwake, majuz usiku kama kawaida tuliongea mpaka mida ya saa 9 usiku ktk maongezi yetu ghafla ikatokea saut ya mwanamke yenye mahaba kama vile anagegedwa huko alipo, tulikaa kimya kama sekunde chache tunahamaki mara akakata simu,mi nikashangaa nikamtumia sms anipigie maana simu yangu ilikwisha hela usiku ule alivyonipigia kaniambia kuna mwanaume mpangaji mwenzie anaishi nae huko alipopanga amemgongea mlango mi nikashangaa mbona hakuna mahusiano na sauti niliyosikia akanijibu nitakuhadithia kesho,kesho ikafika nikamwambia aniambie amekataa na kuanzia hapo alikuwa hanipigii simu wala kutuma sms nikimpigia au nikimwindikia sms hajibu vzuri na mawasiliano amepunguza na hataki kunihadithia nini kilitokea,jaman najua huku jf kuna mabig thinker naomben mawazo yenu,ushauri wenu na maoni mnakaribishwa wote asanteni
 
mh isijekuwa ni msagaji huyo :shock: hio sauti ya mwanamke ya kimahaba inanipa mashaka.
 
Mkuu ukiona manyoya, ujue kaliwa huyooooo! Kusoma hujui sawa, lakini sasa hata picha pia huoni?
 
duh... uhadisiwe nini bwana!? muda wote unabembeleza wenzio wanagonga, achana nae..
 
wewe ni mwanaume au mvulana?kama ni mwanaume acha kutuaibisha wenzio,unataka tukushauri kitu gani?hapa hakuna jibu sahihi utakalolipata,yote ni labda tu!
Anyway,labda ni msagaji,so mfanyie councelling kama kweli umependa,atarudi tu relini,labda anafanya hvo kwakuwa aliumizwa na mwanaume as u said above
 
Back
Top Bottom