Bora mturudishe Must I

mdesi

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
1,366
2,202
Tanzania inayotiririka maziwa na asali sasa imekuwa chungu kama siki! Afadhali turudi tulikotoka kuliko kwenda tusikokujua.
Habari sasa ni kwa wale wenyenazo wanaoweza nunua vifurushi sisi extreme poor people tunalazimishwa kutazama tbc kwani ndo chanel pekee free iliyobaki
Ajira hakuna tena kama tulivyokuwa kule Misri kwa nini mmetuleta jangwani? Tumewakosea nini?
Tuliweza kuwaona na kuwasikiliza wawakilishi wetu wakiwa bungeni lakini huku hakuna, hata tuliokuwa hatuna vyombo vya eletroniki wabunge wetu waliitisha mikutano kuskiliza matatizo yetu lakini huku wamesema tutawasikiliza mnamo mwaka 2020 kwa wale watakao kuwa hai.
Kila mtu anahofu ya vibishara tulivyokuwa vinatusaidia kujikimu vimekuwa vigumu kila mtu anasema pesa hakuna zimeenda wapi? Hadi washroom sasa tunalipa kodi hakika ni bora turudisheni Misri
 
Back
Top Bottom