basha unguja
Member
- Sep 28, 2016
- 83
- 77
Wasalamu!
Hahahah, jamani hii dunia haiishagi vituko asee, jana katika pita pita zangu nimekuta sehemu kunazogo kinoma, kama mujuavyo kwenye zogo hapakosagi mashilawadu, mashilawadu wakawa wanafunguka eti, kuna jamaa anakamchepuko kake ambaye ni baamedi sasa issue iko hivi, huyo madada ni baunsa flani hivi, kiasi kwamba wadada wa maeneo hayo woote wanamuogopa kinoma na siyo wadada tu hadi baadhi ya vidume anavimudu, kutokana na hali hiyo yule jamaa anapelekwa pelekwa kinoma na huyo manzi.
Sasa jana jamaa baada ya kuona manyanyaso yamezidi akaamua kutoa yake ya rohoni, akawa anafunguka kwa kujutia kwa nini alimtongoza dada huyo kwa kuwa hana amani kabisa, kiasi kwamba kwake imekuwa kinyume, amani anaipata kwa mke wake na vurugu zoote anazipata kwa mchepuko jambo ambalo ni kinyume na matarajio yake, Ikitokeea akihudumiwa na mdada mwingine hapo baa huo mchepuko una maindi kinoma noma, akicheka na wadada wengine mchepuko unakuja juu ka moto wa kifuu.
Sasa jamaa akawa anamkataa mbele za watu kuwa kuanzia jana yeye hamtaki tena na mahusiano yafe rasmi, jibu alilolipata kutoka kwa mchepuko ni kuwa pamoja na jamaa anamkataa ila yeye bado anampenda tena sana na bado zamu yake ya kumkataa haijafika hivyo akaomba watu walipuuze ombi la jamaa huyo kuwa ni batili kwa kuwa bado wanapendana na mchepuko kuahidi kuwa ataendelea kudeal naye kama mpenzi wake wa kila siku.
Jamaa kusikia hivyo akaanza kulia kwa sauti kiasi cha kujutia na kusema anatamani akamwambie hata mke wake na amuombe radhi mke wake kwa jinsi anavyokoseshwa raha na mchepuko huo manake alitegemea kupetiwa petiwa kwa unyenyekevu lakini imekuwa kama wako depo ya kijeda vilee, au kama vile yuko mateka flan hivi ameziing! Jamaa mpaka anaondoka akasindikizwa na neno kutoka kwa huo mchepuko, "kapumzike baba see you kesho baby, love you so much" huku jamaa kwa jazba na hasira kaiondoka eneo hilo ka Faru aliyejeruhiwa na bunduki.
Hii michepuko bhana siyo kabisa bora kubaki njia kuu, manake jamaa kachepuka kafika sehemu kakuta daraja limebomoka hakuna kwa kupita imebidi arudi tu njia kuu.
My Take: TUZIHESHIMU NDOA ZETU. TUWAPENDE SANA WAKE ZETU SI TUMEWACHAGUA WENYEWE LAKINI TENA KWA VIAPO KEDEKEDE. NDIYO WAMESHAKUA WAKE ZETU TUWAPENDE SANA TENA SANA KUEPUSHA MATATIZO YASIYO NA ULAZIMA ASEE!
Asante!