Bonifasi Ndengo mfupa uliomshinda mkuu wa mkoa Mara,mkuu wa wilaya pamoja Kassimu Majaliwa

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Ni zaidi ya mwaka sasa tangu Waziri mkuu Mh Kassimu Majaliwa atoke mkoani Mara kwa ziara ya kikazi mkoani humo.

Akiwa Mkoani Mara tena Wilayani Musoma,Waziri Mkuu alipokelewa na mabango ya wananchi wakilalamikia Chama chao cha ushirika kugeuzwa kampuni binafsi na kuibiwa mamilioni ya hela.

Wananchi wa Musoma Mjini walalamikia chama chao cha ushirika kijulikanacho kwa jina IMARA SACCOS LIMITED KILICHOPO karbu kabsa na ofisi za mkuu Wilaya ya Musoma Mjini.

Wananchi walimlalamikia Mh Waziri Mkuu kuwa chama chao cha ushirika kina bwana mmoja aliejigeuza Meneja na yeye ndo mwenyekiti wa chama shemeji Yake na Mbunge wa Musoma mjini. Ndgu Bonifasi Ndengo kuwa amewaibia wanachama wa chama hicho zaidi ya mulioni 60m.

Baada ya malalamiko hayo,waziri mkuu akiwa mkoani Mara,na wilaya ya Musoma Mjini kwenye mkutano wa hadhara ndipo alipo elekeza kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Musoma kumkamata Na kumweka chini ya ulinzi Mtuhumiwa huyo.

Bahati nzuri wakati agizo ilo linatolewa Mtuhumiwa huyo alikuwepo kwenye mkutano huo, na baada ya agizo la Mh waziri mkuu yule bwana alitoka pale amekimbia na police walimuona ila walimuogopa mtuhumiwa na si AGIZO la Waziri mkuu.

Baada hapo waziri mkuu alimwagiza K/mrajisi wa mkoa kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo.

Bahati nzuri wakati Mh waziri Mkuu akitoa agizo la kufanyika uchunguzi,k/mrajisi wa mkoa wa Mra alitekuwepo alikuwa ameisha fanya uchunguzi na kutokana na uchunguzi kuonesha ubadhilifu mkubwa zaidi ya milioni 89m ziliibwa na Mtuhumiwa yule Bonifasi Ndengo, alishachukua hatua za kumsimamisha uongozi.

Pamoja na hatua kuchukuliwa ikiwemo Takukuru mkoa wa Mara kuchunguza, BONIFAS ndengo ni mwaka wa 3 hajawai kukamatwa,yupo mitaani vuongozi wa mkoa wa Mara wamebakia kurushiana mpira ukimuuliza Mkuu wa wilaya anasema anasubiri Takukuru wamfungulie mashitaka,

Ukimuuliza kamanda takukukuru,mkoa anakwambia faili liko kwa DPP,ukimuuliza mkuu wa mkoa ambae aliwai kuitisha kikao na viongozi wa chama na mbunge wa musoma mjini na kuaidi kuchukua hatua pale unaambulia matusi.

JE BONIFADI NDENGO NI NANI MKOANI MARA?

1.NI KADA WA CHAMA CHA MAPINDUZI,aligombea Uraisi kupitia kura za maoni.

2. Ni shemeji wa Mbunge wa Musoma mjini, mbunge kabla ya kuwa mbunge aliitisha mkutano mkuu wa imara saccos ltd na kuaidi kuwapa wanachama 200m kama ruzuku baada ya kupewa kura aliingiza fedha hizo ila kilichitokea shemeji shemeji washa taaa.

3.ALIKUWA MWENYEKITI/MENEJA WA IMARA SACCOS LTD,NA KUIPANGISHA KWENYE JENGO LAKE KILA MWEZI CHAMA KILIKUWA KINALIPA 2M mkuu wa mkoa alivunja mkataba na kuagiza chama kiame.

4.MWENYEKIT CHAMA CHA WAFANYA BIASHARA MARA.

JE vyeo hivi ndo vilifanya mkuu wa mkoa wa Mara na mkuu wa wilaya washindwe kutekeleza agizo la Waziri Mkuu?
 
Mkuu hii imekaa kishabiki shabiki. Unajuaje kama alishakamatwa na akadhaminiwa? maana dhamana ni haki ya mtuhumiwa. siyo kwamba waziri mkuu akisema mtu akamatwe hapatagi dhamani
 
Mkuu hivi sasa kuna sera ya lipa utoke

Nakushauri fuatilia vyema pengine kijana walishafunga na acc zake akajisalimisha yakaisha

Hivi sasa hatutangazi tena kwa usalama wa watuhumiwa so DPP akipokea maombia mkakubaliana mnamalizana tunatengeneza barabara zetu.

Sio kujaza watu jela wanakula bure tunaishia kuitia hasara Serikali
 
Mengine siyajui sana ila najua mwaka kama sikosei 1999 nilishiriki katika igizo na ngonjera ya kumpongeza huyu bwana kwa kufaulu kujiunga na chuo kikuu dar akitokea kijijini kwetu na leo ndio nasikia hbari zake
 
Back
Top Bottom