Boniface Jacob(Boni Yai): Nakulilia rafiki yangu Mdude

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
33,615
Reaction score
40,162
NAKULILIA RAFIKI YANGU MDUDE

Ni siku takribani 8 tangu uvamiwe, utekwe, ujeruhiwe na kupotezwa ukiwa ndani ya nyumba yako kata ya Iwambi, Jijini Mbeya.

Tukio lako limeacha maswali mengi bila majibu, simanzi kubwa kwa ndugu, Jamaa na familia yako.

Nilichofanikiwa kujua hadi sasa ni kimoja tu, kwamba kabla hawajafanikiwa kukudhibiti na kutoweka na wewe, ulipambana kwanza mpaka ulipozidiwa nguvu.

Damu yako kumwagika ni ishara ya kupata majeraha makubwa katika mwili wako, michuruziko ya damu ni ishara ulichukuliwa na watu wakatili sana.

Kukosekana kwako hadi sasa ni ishara kwamba waliokuteka ni watu wenye taaluma na wajuzi wa medani za mapigano katika misheni mbalimbali kwa maelekezo maalum.

KUMBUKUMBU;

Nakumbuka mara ya kwanza nilipoonana na MDUDE uso kwa uso ofisini kwake Mbozi, mkoa wa Songwe.

Nikiwa Diwani wa Kata ya Ubungo nilikuwa nimetumwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwenda Mbozi kusimamia mechi ya timu yetu ya daraja la kwanza ya KMC.

Wakati ule ilikuwa bado inaitwa TESEMA msimu wa 2013/14 tulinunua kutoka TEMEKE kwa mtu anaitwa Ndonga lakini tukachelewa kubadili jina kuwa KMC

Nakumbuka msafara wa timu uliongozwa na mimi pamoja na Sharif Majisafi (alikuwa Diwani wa kata ya Bunju, CCM) tulikuwa tumetumwa sisi kwa sababu mbili..

Sisi wawili ndiyo tuliasisi vikaoni wazo la halmashauri kumiliki timu daraja la kwanza ili baadae ije kupanda hadi ligi Kuu.

Sababu ya pili timu ya KMC (TESEMA) ilikuwa imeshapoteza michezo zaidi ya 5 bila pointi hata moja, tulitumwa Mbozi kuhamasisha timu na kujifunza changomoto za ligi daraja la kwanza.

Asubuhi mapema kabla ya mechi nilimkuta Mdude katika fremu za soko, nje ya stendi ya Mbozi, Duka lake dogo la simu na vifaa vya umeme, akiwa na suti nyeusi, mrefu nadhifu lakini jasiri na mwenye kujiamini.

Mchana niliachana na Mdude nikaenda uwanjani, kwa bahati siku hiyo timu ya KMC (TESEMA) ilikuwa inaongoza mchezo kwa goli moja

Lakini Kwa bahati mbaya mechi ya KMC Vs KIMONDO haikumalizika kwa sababu ya mvua kubwa dakika ya 80.

Refa alimaliza mpira na viongozi wa timu zote mbili tuliitwa ofisi ya ya chama cha soka wilaya ya Mbozi ili mchezo urudiwe kesho yake asubuhi kumalizia dakika 10 zilizobakia.

Si unajua mizengwe ya mpira tena, kule ofisini kamisaa na refa wakasema mpira haukusimamishwa dakika ya 80 bali dakika ya 50. kwa hiyo kesho asubuhi, zitarudiwa dakika 40 na siyo dakika 10.

Jamaa walikuwa serious kweli, timu ya wapinzani wetu KIMONDO FC ilikuwa inamilikiwa binafsi na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mbozi (CCM)

VURUGU

Katika kubishana na kutetea haki yetu ya KMC (TESEMA) nikaanza kutukanana na viongozi wa mpira wilaya ya Mbozi baadae mmoja akanitemea mate pale ofisini na Polisi wakiwemo.

Si unanijua kwa utata? Ndugu yenu nikapanda juu ya meza nikamrukia kwa kichwa yule kiongozi wa mpira wa Mbozi.

Basi kikanuka mbaya, lakini sisi tupo wachache sana na Jamaa zetu wapo nyumbani na ni wengi sana, Jamaa nikiwa nimekabana kabari na yule kiongozi ukutani, mgongoni nilihisi ngumi nyingi sana kutoka kwa wenzie.

MDUDE ndiyo aliingia mlangoni kwa teke, mlango uliokuwa umerudishiwa kwa komeo la ndani ili washabiki wasiingie ndani.

Support ya Mdude ilikuwa kama msaada kutoka kwa Malaika, nikajikuta nimepata nguvu upya na mashambulizi yakapungua kwangu baada ya kuwa vichaa wawili mule ndani, tukawa tunarushiana viti mpaka polisi walipotutuliza.

RAFIKI WA KWELI

Nilimpenda Mdude tangu siku hiyo nakumbuka baada ya ugomvi mashati yetu yamechanika ndiyo Mdude ananiuliza chanzo cha ugomvi.... What a friend...?

Anasema alipoambiwa rafiki yako (Bonge) aliyekutembelea ofisini asubuhi wanamchangia ofisi ya chama cha mpira katika fremu za uwanjani

Mdude aliita vijana wake wa CHADEMA pale stendi haraka sana wakaja kunisaidia ugomvi bila kujua chanzo cha ugomvi.

NAMBA 4

Namba ya 4 ndiyo Jina la utani tunaloitana mimi na MDUDE ni baada ya kuishi Gereza la Ruanda, Mbeya aliniadithia kuhusu vituko vya selo namba 04 ambayo walikuwa wanaishi watu wenye matatizo ya akili (vichaa)

URAFIKI

Ulikolea zaidi 2016 baada ya Mdude kutekwa 26 August 2016 mara ya kwanza na kuletwa Dar es salaam 01 September 2016.

Baada ya kupewa mateso ya kupigwa uume (penis) kwa fimbo na rula na wadada waliokuwa wanamtesa hadi kukojoa damu baada ya kuachiwa mateka

Nakumbuka nilimlipia gharama za matibabu ya hospitali mbalimbali za Dar es salaam hadi kupona.

MIKASA YA MDUDE NA DOLA

Agosti 26, 2016 - Mdude alikamatwa Vwawa, Mbozi

Agosti 28, 2016: Mdude alihamishiwa kambi ya FFU Mbeya

Agosti 29, 2016 - Mdude alipelekwa Dar es Salaam na kuwekwa Oysterbay polisi.

Septemba 1, 2016: Mdude alipelekewa hospitali ya Mwananyamala Dar Es Salaam kufuatia madai ya kuteswa.

Septemba 13, 2016 - Polisi wamuondoa Mdude hospitali Mwananyamala na kumpeleka Vwawa.

Septemba 14, 2016 - Mdude alifunguliwa kesi ya mashtaka ya kuandika uongo.

Aprili 15, 2017 - Mdude ashinda kesi.

Novemba 2017: Mdude alikamatwa tena Vwawa na kupelekwa Dar Es Salam ambako aliwekwa kituo cha Polisi cha Central kwa siku 21.

Baada ya hapo arudishwa Vwawa ambako afunguliwa kesi ya uchochezi

Novemba 2018: Kwa mara nyingine Mdude ashinda kesi Novemba 2018.

Januari 2019: Mdude aandika notisi ya kulishtaki Jeshi la polisi

Juni 28, 2021; Mdude aachiwa huru na kushinda kesi ya Kusafirisha Madawa ya kulevya.

Machi 2019: Mdude alifungua kesi mahakama kuu kanda ya Mbeya na kumshtaki Inspekta Jenerali wa polisi, RPC wa Songwe, Mwanasheria mkuu wa serikali na askari polisi watatu.

Julai 14, 2023; Mdude ashikiliwa na Jeshi la Polisi Mbeya

Julai 17, 2023; Mdude aachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi Mbeya

August 12, 2023; Mdude na Mwabukusi wakamatwa Mikumi wakiwa safarini kwenda Dar es salaam.

November 22, 2024; Mdude na Viongozi wengine akiwemo Mbowe alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Songwe.

December 06, 2024; Mdude aachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi.

May 02, 2025; Mdude anavamiwa nyumbani kwake Mbeya na kutoweshwa kusikojulikana.

Nakulilia rafiki yangu MDUDE.
 
20250511_090923.jpg
 
Duh huu mtiririko wa hii habari hadi unaliza, nawaza tu je hao watesi wao hawataonja mauti? Na kama wataonja yatakuwa ya namna gani?
 
Msituchoshe maandishi marefu sana!
 
Back
Top Bottom