Kabisa king sasa hii yasababishwa na nini???
Kuna mastaa Bongo? Huwa najiuliza mara nyingi swali hili nisikiapo watu wakijiita mastaa. Sidhani kama kuna staa (kwa maana halisi ya ustaa) yeyote hapa Bongo. Nitajieni mmoja ili nimchambue. Eti mtu akiingia kwenye uigizaji wa filamu za ajabu ajabu zisizo na mbele wala nyuma tayari anajiita staa. Wenzetu kule Ulaya mastaa ni watu wenye mafanikio makubwa katika fani zao na tayari wametengeneza fedha za kutosha, na wanajulikana kimataifa kutokana na weledi wa kazi zao.