Bongo Movie Vs Bongo Flavour.

Qunax

Senior Member
Oct 16, 2016
100
127
Miaka ya nyuma vijana wengi ilikuwa tukienda Club zikipigwa ngoma za dancehall za kina Sean Paul na ngoma nyingine nyingi za mbele ilikiwa tunaruka zaidi kuliko za Bongo lakini wasanii wa bongo na maproducer wao kama kina P-funk, Loy wa G2,Mika Mwamba,Enricko waliamua kufanya yao na wabongo wakaacept mziki wa bongo nao ukawa na Soko mpaka leo hii mziki uko pazuri na unalipa club gonga nyimbo za mbele ila usipogonga ya Shilole, au Singeli watu hawakuelewi hata kasi ya vijana kusikiliza ngoma za mbele, sijui bolingo imepungua,Watu wanasikiliza mziki wa nyumban coz wapo wasanii kutoka nyumban wanaofanya vyema.
Hii iwe funzo kwa bongo movie wakae wajipange watoe vitu tofauti watu watakubali tu, ni vigumu sana kunishawishi niache kuangalia prison break niangalie "teke la mama" Na hii ndio inapelekea raia wengi kumkumbuka Marehemu Kanumba na kuamini ni yeye tu laiti kama angekuwepo mpaka leo ndiye ambae alikuwa na uwezo wa kuwateka watazaji wa filamu wa hapa nyumbani.....
Pia wasanii wa Bongo movie kuweni watu wa kazi punguzeni kuuza sura, wasanii warembo wa Hollywood kama kina Lucia hatujawasikia hata kwenye majarida,Yusuph mlela na Hemed ni kweli mzee mna body nzuri ila body zenu sio kama za kina Rambo,Anold, Van Dame, Sharkan au Ramseh Noah, ila wale wenzenu sio watu wa mauzo ni watu wa kazi.
Nakumbuka marehemu Kanumba kabla hajafa kuna siku alisema wasanii wadada Watanzania wananenepeana tu na kupoteza mvuto, wale wasanii wadada wakaja juu sana na kumtukana jamaa lakin leo hii ni kweli ukimchek @Tea,Wolper,Wema hawajulikani kiuno kiko wapi tumbo liko wapi.
Na kingine pia industry ya bongo movie haiendani na ukweli, unakuta movie producer JB, director JB, script writer JB, Story JB na Starring JB, ni uongo, kuna watoto wengi nowdays wamesomea video editing and graphics wako huko mitaan hapa hapa kwetu wanaedit katuni na kupost instagram hawana kazi wanajua kutumia hayo maadobe photoshop wapeni nafasi.
Na urembo wa mtu, uhandsome au kuwa na matako makubwa kisiwe ndio kigezo cha kuwa actress au actor, mbona Samuel Jackson sura yake haonekani akiwa anacheka anakuwaje na akilia anakuwaje na msanii mkubwa duniani?

NB: Kitu ambacho watanzania tunafanya dhambi kubwa kwenye bongo movie ni kutoamini ukweli ambao upo tangu miaka ya 90 juu ya Bongo movie, I swear comedian wa Bongo wamedo the Best ila tatizo tumewapotezea sana ila hawa jamaa atleast. Big up mzee Majuto,Kingwendu,Joti,Max,Zembwela,Mizengwe nk.

Kuweni seriuz tutafika.
 
Back
Top Bottom