Ujasirinimtaji
Member
- May 3, 2016
- 18
- 10
Kwanza natoa pongezi kwa raisi wetu kuhakikisha mapato na matumizi ya nchi kwa kila mwezi huwa yanatolewa hadharani ingawa mwezi huu taarifa yake imechelewa ila ni matumaini yangu itakuja soon,
Kikubwa kwenye uzi huu ni kuonesha jipu linaloanza kuchomoza katika chuo cha usafirishaji (NIT) na bodi ya mikopo kwa kushindwa kuwapatia wanufaika wa mikopo wanaoendelea na masomo yao huku hela ikiwa imeshatolewa n serikali tokea bajeti ya mwezi wa tatu, fedha hizi zimeshafika bodi ya mikopo tatizo lipo kati ya taasisi hizi mbili bodi na chuo cha usafirishaji kwa kushindwa kuwapatia wanafunzi pesa zao kwa makusudi na kuwaacha watoto wa watanzania masikini wakisoma kwa shida na tabu bila ya kuwa na mtu wa kuwasaidia kwani hadi mkuu wa chuo hajaweza kuchukua hatua zozote mpaka sasa wala bodi ya mikopo haijawa tayari kutulipa pesa zetu.
Ikumbukwe mwaka jana bodi ya mikopo ilichakachua pesa za wanafunzi za field wakisingizia hawakupata barua ya maombi ya pesa hiyo kutoka chuo na mwaka wa fedha wa bodi ukawa umeisha, naona na mwaka huu tena wanashindwa kusoma alama za nyakati kwa kujua hizi ni zama mpya na raisi wetu mh Magufuli hawezi kukubali fedha zinazopelekwa na serikali kuwasomesha watanzania wanaotoka katika familia masikini hawanyanyaswi kwa namna yoyote ile.
Ombi langu kwa raisi, wziri wa elimu na wa fedha ni kutuma task force ikachunguze watu waliokula hela ya Field mwaka jana na ni nani anayechonga huu mchongo mpya wa kutaka kutakatisha fedha za wanafunzi za quter 3 ambazo mpaka sasa wanafunzi wanalia njaa kwani hali za wanafunzi ni ngumu sana.