Anicet mchomvu
Member
- Apr 18, 2012
- 95
- 213
UKISIKIA KWAMBA MWENDOKASI BILA UMAKINI UNAUWA ..BASI
KUUWA KWENYEWE NDIO HUKU...
BODI YA MIKOPO/HESLB...
Kwa mujibu wa Bw. Badru, kundi la kwanza linajumuisha wanafunzi waombaji wa mikopo wenye uhitaji maalum kama wenye ulemavu uliothibitishwa na Waganga Wakuu wa Wilaya na yatima ambao katika maombi yao waliwasilisha nakala za vyeti vya vifo zilizothibitishwa na makamishna wa viapo.
“Kundi la pili linajumuisha waombaji wa mikopo ambao baada ya uchambuzi wa taarifa zao walizowasilisha na baada ya kulinganisha na gharama za jumla za masomo yao ya sekondari, wamebainika kuwa wana uwezo mdogo wa kugharamia masomo yao ya elimu ya juu na hivyo kuwa na uhitaji zaidi wa mikopo,” amesema Bw. Badru.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bw. Badru ametaja kundi la tatu na la mwisho kuwa linajumuisha waombaji wa mikopo ambao wenye ufaulu wa juu katika matokeo yao ya kidato cha sita na wamechaguliwa kujiunga na fani za kipaumbele kwa taifa.
Fani hizo ni Sayansi za Tiba, Ualimu wa Sayansi na Hisabati, uhandisi wa Kilimo, Mafuta na Gesi na Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
Makundi ya wanafunzi waliopata mikopo
“Hivyo basi, hadi sasa tumetoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 wakiwemo wanafunzi yatima 4,321, wenye ulemavu 118, wanafunzi wenye uhitaji waliosomeshwa na taasisi mbalimbali katika masomo ya sekondari (87), wanafunzi wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159 na wanafunzi wanaosoma kozi zisizo za kipaumbele lakini wanaotoka kwenye familia duni 9,498,” amefafanua Bw. Badru.
Sababu za kukosa mikopo
Katika mkutano huo, kiongozi huyo wa HESLB pia ameeleza kwa kina sababu nyingine za waombaji 27,053 ambao hawajapangiwa mikopo.
Ametaja sababu hizo kuwa ni pamoja na baadhi ya waombaji (90) kuwa na umri wa zaidi ya miaka 30, waombaji mikopo waliopata udahili kwa sifa linganishi (equivalent qualifications) na waombaji waliomaliza masomo ya kidato cha sita zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
Kundi jingine la waombaji waliokosa mikopo katika awamu ya kwanza ni waombaji waliopata nafasi katika vyuo kwa ufaulu wa mitihani waliyofanya kama watahiniwa binafsi (Private Candidates) na waombaji ambao hawakurekebisha fomu zao za maombi ingawa waliitwa kufanya hivyo.
Nafasi ya rufaa na uhakiki wa wanafunzi wanaoendelea na masomo
Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji huyo pia amewataka waombaji ambao hawajaridhika na upangaji wa mikopo unaotangazwa, kuwasilisha rufaa zao kwa njia ya mtandao utakaofunguliwa kuanzia katikati ya wiki ijayo.
“Tunafahamu kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wamekosa mkopo kwa kutowasilisha baadhi ya nyaraka ingawa tuliwaomba kufanya hivyo, hawa na wengine wenye sababu za msingi, watapata fursa ya kuwasilisha rufaa zao kwa njia ya mtandao na nakala kuzituma kwa utaratibu tutakaoutangaza wiki inayoanza kesho,” amesema Bw. Badru.
KOSA MLILOFANYA NI KUWACHELEWESHEA MIKOPO AMBAPO WENGI WA WANAFUNZI WAMESHARIPORT NA KUANZA MASOMO HUKU WAKITARAJI KUPEWA MIKOPO........
ALAFU LEO UNAMUAMBIA HANA SIFA ZA KUPEWA MKOPO ETI KWA SABABU ZISIZO NA MASHIKO KAMA HIZO APO JUU UNAFIKIRI KITU GANI KITAENDA KUTOKEA BAADA YA TAARIFA HIZOO.. KAMA MWANZONI MLIVYOLETA UTARATIBU WENU WA MEAN TEST KUKAWA VILE...
Huku bosi wenu akishindwa kujieleza vizuri huku akijing'atang'ata eti ooo mara bodi mnafanya kazi kwa mazoea mara kama ni ivoo bora wasipewe n.k ALAFU LEO MNAKUJA NA UPUUZI MWINGINE HUO?? HAKIKA BODI MJIANDAEE MSIMU HUU ITANYESHA MVUA NA SIO RASHARASHA ZA UD TENA ,,
MTAISOMA NAMBA....