Bodi ya Mikopo kimeeleweka, pressure Hakuna

Bodi ya Mikopo kimeeleweka, pressure Hakuna

must be

Member
Joined
Oct 6, 2014
Posts
84
Reaction score
28
Hatimaye bodi ya Mikopo imeweka mambo hadharani baada ya kimya cha muda mrefu

TAARIFA KWA WAOMBAJI WA MIKOPO KUHUSU KUMALIZIKA KWA ZOEZI LA KUREKEBISHA TAARIFA ZA WAOMBAJI

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekamilisha zoezi la kurekebisha fomu za maombi ya mikopo kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Zoezi hilo lilianza tarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Oktoba 2016.

Kwa sasa Bodi inaendelea na hatua za awali za upangaji wa mikopo ambapo taarifa za wanafunzi watakaopangiwa mikopo zitatolewa kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz siku chache zijazo.

NB: Bodi inawakumbusha waombaji mikopo wote kuwa makini na watu wasio waaminifu wanaoweza kutumia fursa hii kujipatia fedha isivyo halali.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
 
duh mimi nikajua wameshaanza kutoa,kumbe unarudia mambo ya juzi...
 
Huku bado wengine tupo kwenye list ya waliokosea wakati tusharekebisha na simu zao hawapokei
 
Back
Top Bottom