Bodaboda & armed robbery

Prosper C Manasse

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
635
690
My OUTLOOKS
* * * * * * *
06/MARC/2016

BODABODA & ARMED ROBBERY:
Biashara Ya Usafirishaji Abiria Kwa Bodaboda Ni Biashara Ambayo Imeshamiri Sana Tanzania Kwa Takribani Miaka Mi5 Hadi7 Sasa.

Sekta Hii Isyo Rasmi, Imeajiri Vijana Wengi Sana Na Serikali Pia Inatambua Mchango Wao Kwa Kuwapa Maeneo Ya Kufanyia Biashara Hiyo Licha Ya Changamoto Za Hapa Na Pale.

Jambo Ambalo Ni Baya Zaidi Ni Pale Ambapo Baadhi Ya Watu Wamekuwa Wakitumia Mwanya Wa Aina Hii Ya Usafiri Kufanya Vitendo Vya Kihalifu.

Tumeshuhudia Na Kusikia Kwa Ndugu, Jamaa Na Marafiki Jinsi Walivyonyang'anywa Pesa Zao Na Watu Ambao Hutumia Pikipiki.

Matukio Ya Aina Hii Yamejitokeza Mara Kadhaa Na Kuripotiwa Likiwemo Tukio La Hivi Karibuni La Uvamizi Wa Bank Eneo La Mbagala Ambapo Tumepoteza Askari Wetu Wazalendo Wakat Wakipambana Na Majambazi.
Mungu Azilaze Roho Zao Mahali Pema Peponi.

Zipo Njia Kadhaa Ambazo Zimefanywa Na Jeshi La Polisi Ili Kupunguza Na Kuzuia Kabisa Aina Hii Ya Uhalifu Lakn sote Tunafahamu Kwmb Wahalifu Ni Watu Ambao Hukesha Kupanga Njia Nyingi, Mpya Na Jinsi Ya Kukamilisha Na Kufanikisha Matukio Yao.

Moja Kati Ya Njia Ambayo Imesaidia Kwa Kiasi Fulani Ni Kuzuia Pikipiki Kuingia Katikati Ya Mji Ambako Taasisi Nyingi Za Kifedha Na Ofisi Mbali Mbali Zipo Huko.
Japo Njia Hii Inalaumiwa Na Watu Wengi Ikiwemo Bodaboda Ambao Pengine Wanania Njema Tu Ya Kufanya Biashara Yao Vizuri Lakn Ni Vyema Tukatambua Licha Ya Sababu Ya Kuzuia Uhalifu Zipo Sababu Nyingine Nyingi Za Kwanini Bodaboda Wasiingia Katikati Ya Mji.

JINSI WANAVYOFICHA SILAHA.
Wakiwa Wanaenda Kufanya Tukio Huwa Huvalia Makoti Makubwa Kiasi Na Kuficha Silaha Zao Humo. Ukimwona Na Koti Unaweza Kufikiri Ni Bodaboda Kumbe Ni Muhalifu Sugu. Wataingia Sehemu Husika Kama Wateja Na Hapo Ndipo Hufungua Zipu Ya Koti Na Kukuonyesha Silaha Huku Wakitamka Maneno Ya Vitisho.

Hata Kwa Wale Wanaotoka Kuchukua Fedha Bank, Wakikupa Maelezo Ya Tukio Watakwambia Wanakutana Na Mitego Hii Hapa.

1. Upo Kwny Gari Yako Unatoka Bank Au Kwny Mauzo/Makusanyo Ya Fedha.

2. Ghafla Watu Kadhaa Wanakuja Na Pikipiki Eidha Kwny Foleni Au Wanakuvuzia Sehemu Ambayo Hakuna Watu Wengi.

3. Wakat Wewe Huna Hili Wala Lile, Jambazi Aliyepakiwa Nyuma Ya Pikipiki Anafungua Koti Na Kukuonyesha Silaha Kifuani Mwake Huku Akiwa Ameshaitoa.

4. Wakat Unaendelea Na Safari Yako, Mmoja Anakupa Amri Ya Kusimama Vinginevyo Afanye Anachofanya.

5. Wahalifu Huchukua Mzigo Na Kutokomea.

Hili Tendo Hufanyika Kwa Haraka Sana Kiasi Kwmb Hata Mliokaribu Mtakuja Kujua Wakati Tukio Limeshafanyika.

USHAURI WANGU KWA MANISPAA ZOTE TANZANIA PAMOJA NA JESHI LA POLISI.
1. Itungwe Sheria Ndogo Ktk Majiji Ambayo Itaweza Kutofautisha Kati Ya Waendesha Bodaboda Na Pikipiki Binafsi.

2. Bodaboda Wawe Na Sare Maalumu Ili Watambulike Na Kila Mtu, Na Pia Wajisajili Ktk Vituo Vyao. Hii Itasaida Ktk Kuwatambua Wahalifu Kwa Haraka Hata Kama Wahalifu Ni Baadhi Ya Bodaboda.

3. Itafutwe Namna Kwa Bodaboda Na Wamiliki Wa Pikipiki Binafsi Ambapo Hawatoruhusiwa Kuvaa Makoti Makubwa Waingiapoa Bank Na Ktk Taasisi Nyingine Za Fedha Kwa Hofu Ya Kuficha Silaha.

NB. Sababu Nilizotaja Zinaweza Zisijitosheleze Lakn Zikasaidia Ktk Ulinzi Na Usalama, So Sisi Wananchi Kama sehemu Ya Ulinzi Na Usalama Bila Kuwasahau Viongozi Wetu, Tunaweza Kupunguza Ama Kuongeza Nyama Ktk Ushauri Niloutoa Kwani Sote Dhumuni Letu Ni Moja Tu "Kuzuia UHALIFU".

HITIMISHO:
Sisi Sote Tunaathiriwa Na Vitendo Vya Kihalifu Kwa Namna Moja Ama Nyingine, Jambo Ambalo Tunatakiwa Kulitambua Na Kulifanya Sasa Sisi Ni Hili hapa.

a) Kila Mmoja Wetu Kwa Utashi Wake Na Nafasi Yake Ktk Jamii, Anaweza Kutoa Ushauri Kupitia Jukwaa Hili Ili Ujumbe Na Ushauri Wake Uwafikie Walengwa Ili Sote Kwa Pamoja Tuweze Kufanya Biashara Zetu Kwa Amani.

b) Yapo Masanduku Ya Maoni Ktk Ofisi Za Kijiji, Mkuu Wa Wilaya/Mkoa, Unaweza Kuandika Maoni Yako Ukayaweka Pale Kisha Kamati Ya Ulinzi Na Usalama Ikayapitia.

c) Baadhi Ya Watu Wana Access Ya Kukutana Na Viongozi Kutokana Na Mazingira Wanayoishi Au Wanayofanya Kazi, So Ni Vyema Tukawapa Michango Yetu Aral Or Written Ili Waifikishe Mahala Husika.
Hii Itasaidia Usalama Wa Taifa Letu Kuhimarika Sana Badala Ya Kukaa Na Kulaumu Bila Kutoa Maoni Kwa Walengwa Huki Tukiendelea Kuumia.

TUKIACHA LAWAMA NA KUTOA USHAURI, KWA PAMOJA TUNAWEZA KUTOKOMEZA UHALIFU. MIMI NA WEWE NI WADAU KTK KULINDA USALAMA WA RAIA NA MALI ZETU, KWA PAMOJA TUNAWEZA.
 
umeongea vizur mkuu ila hapi kwenye sare bado ni changamoto, wale majambazi ya arusha yaliyokamatwa juzu juzi pale yalikua na sare za jeshi, pia kuna ripoti kibao tu za watu kuvaa nguo za kijesh au afisa usalama barabarani na kufanya watakalo, so uniform sio suluhu kabisa yaani.
 
Majambazi wa aina yoyote wakithibitika bila shaka kuwa wametenda uhalifu wa silaha kama ville kuua na kupora pesa au mambo yenye sura hiyo,itungwe sheria ya kuwapiga risasi hadharani barabarani huku watu wakishuhudia ili liwe fundisho kwa wote wanaoshiriki vitendo hivyo au wanaodhamiria kuwekeza katika uhalifu wa aina hiyo. Hii iextend mpaka kwa Bank tellers wanaoshirikiana nao. Hiyo ndio dawa pekee mujarabu ya kutokomeza uhalifu wa aina hiyo maana tumechoka kusikia matukio haya kila kukicha na hawaonekani kuogopa wala kuwa na dhamira ya kuacha.
 
Ni Kweli Mkuu Lakn Bora Ziwepo Kuliko Kutokuwepo Kabisa. Zikiwepo Zitaleta Ugumu Fulan Kwa Wahalifu.
 
Majambazi wa aina yoyote wakithibitika bila shaka kuwa wametenda uhalifu wa silaha kama ville kuua na kupora pesa au mambo yenye sura hiyo,itungwe sheria ya kuwapiga risasi hadharani barabarani huku watu wakishuhudia ili liwe fundisho kwa wote wanaoshiriki vitendo hivyo au wanaodhamiria kuwekeza katika uhalifu wa aina hiyo. Hii iextend mpaka kwa Bank tellers wanaoshirikiana nao. Hiyo ndio dawa pekee mujarabu ya kutokomeza uhalifu wa aina hiyo maana tumechoka kusikia matukio haya kila kukicha na hawaonekani kuogopa wala kuwa na dhamira ya kuacha.
Adhabu Ya Kuuwa Ni Kunyongwa Japo Haki Za Binadamu Zimeingilia Kati.

Kunyonga Ni Nzuri Hata Hawa Wanaokata Viungo Vya Albino Wapigwe Kitanzi Tu.
 
Back
Top Bottom