realoctopus
JF-Expert Member
- May 11, 2014
- 3,232
- 1,982
Wapendwa,habarini za mchana.
Kuna jambo limezuka hivi karibuni,linanipa mashaka kidogo,ni kuhusu hizi boda boda zinazo ondolewa taa ya break ya nyuma(rear light).
Mimi ni mtumiaji mzuri sana wa barabara usiku,ila hili jambo linanipa mashaka sana,kwamba kwa nini piki piki zote zinazo endeshwa usiku hasa hasa na vijana,vijana wenyewe ukiwatizama vaa zao,angalia yao na aina ya iendeshaji wanatisha balaa yaani kama majambazi.
Niliwaza kuwa inawezekana wanaziondoa ili wakikimbizwa usiku baada ya kufanya uhalifu,wasionekane wanapo pitia,maana ukizingatia taa inayo baki wakiendesha ni ya mbele tuu,hivo akiingia chocho akiizima paap,humuoni hata.
Sijui labda ni fikra zangu za kiwoga,au ni hisia za kweli!
Kama wenzangu mmeliona hili,naombeni tushauriane,ili kama lina husika na maovu,tuliombe jeshi la polisi liwadhibiti.
Asanteni.