isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,152
- 6,601
Wengi tunao uwezo wakufanya yote hayo endapo wenye dhamana watatushika mikono na kutuinua.Hivi hawa watu huwa wanaanzia wapi katika ubunifu wao... Wanagundua kitu na kuzodi kukiendeleza.... Waligundua simu za button zisizo na rangi, wakaja ongeza rangi... Wakaja kundua tena smartphone hamna button lakini unabonyeza kitu kina-respond... Hivi sisi hatuna akili ya kugundua? Nawashangaa sana wazungu.
Ubunifu unakuja pale unapokua umeshatatua matatizo yako ya msingi katika maisha, afrika bafo tuna shida nyingi na matatizo kibao, ni aghalabu sana kufikiri kwa ubunifu ukiwa una njaa, maradhi na mafuriko n.k., wenzetu walishamaliza zamani sana...
Indeed! Na bado naamini Afrika uwezo upo lakini uwezeshaji ndio tatizo.Nadhani ubunifu unakuja pale unapokua na matatizo mengi. Matatizo hayo yatapelekea wewe kuwaza njia ya kuyatatua hapo ndio utabuni kitu kitakachokusaidia kutatua matatizo hayo.
Huwezi kuniambia mtu aligundua gari wakati akiwa ameshatatua tatizo la kwenda umbali mrefu kwa kutumia mda mfupi, tatizo hilo la umbali ndio lilipelekea akabuni kitu kitakachosaidia kumsafirisha umbali mrefu kwa muda mfupi.
Njaa, maradhi, mafuriko n.k ilitakiwa tubuni njia ya kutatua/kukabiliana nayo