Blogs za vyama

Blogs za vyama

platozoom

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
9,548
Reaction score
11,517
Najua wakuu wa Vyama hivi wanatembelea JF. Na tunajua teknolojia ya habari na mawasiliano ilivyo muhimu katika kupashana habari, inaweza kuzuka hoja kwamba hii mitandao ya kijamii inatembelewa na watu wachache sana lakini jibu rahisi la hoja hiyo ni kwamba "ni kweli lakini impact yake ni kubwa sana" Juma atasoma na kumhadithia Musa ambaye hajui kutumia mtandao naye atawaeleza wenzake kule walipo . Chain ya mwasiliano itaenda kwa mfumo huo na hatimaye habari zinawafikia wengi.

Nimekuwa napitia mara mojamoja kwenye Blog ya vyama hivi Viwili (CHADEMA na CCM). CCM kwa upande wake wana blog nzuri, ina sehemu ambazo unaweza kusoma historia, katiba na miongozo yao bila kusahau Jumuiya zake.

Lakini hali ni tofauti kwa CHADEMA, ndiyo blog inaonyesha picha za harakati mbalimbali za kisiasa, matukio muhimu pamoja na picha za viongozi wake lakini inakosa vitu vingine vya ziada na muhimu sana kama Katiba, Vision, matamko muhimu ya viongozi , Ilani za uchaguzi zilizopita, hotuba n.k. Ndiyo kuna link ya wavuti lakini ni vyema hayo yote yakawepo kwenye blog pia ambayo ni rahisi kufikika

Ni muhimu kukumbuka kuwa kuna vijana wengi sana wanaingia kwenye mitandao na ni vyema wakapata fursa ya kusoma mambo ya msingi ya kichama ili wawe na mtizamo unaoleweka na pengine "kuwaambukiza" wenzao. Mimi si mwanachama wa chama chochote kile, lakini pengine kwa maoni haya watarekebisha.

Karibuni.
 
Ni kweli mwanzisha mada nafikiri ameshindwa kutofautisha Blog na Website. Hayo yote anayozungumzia yanapatikana katika tovuti (website) ya Chadema. Kumbuka pia CCM wana tovuti na Blog. Kwenye tovuti ndio utaona hayo unayosema na kwenye blog yao hakuna hicho unachokisema. Nafikiri kwa upande wa Chadema unazungumzia Chadema Blog na nyinginezo
 
Jibu swali unajua tofauti kati ya Blog na Web? sema tukurudishe darasani jombaa!

Darasani nilishatoka kitambo. Mimi nimezungumzia Blog sijasema web au niliposema wavuti ukachanganyikiwa (wavuti ni web) ambayo sijakataa kwamba haipo.
 
Ni kweli mwanzisha mada nafikiri ameshindwa kutofautisha Blog na Website. Hayo yote anayozungumzia yanapatikana katika tovuti (website) ya Chadema. Kumbuka pia CCM wana tovuti na Blog. Kwenye tovuti ndio utaona hayo unayosema na kwenye blog yao hakuna hicho unachokisema. Nafikiri kwa upande wa Chadema unazungumzia Chadema Blog na nyinginezo

Naona hatujaelewana kabisa, ni kweli nimeiona website na siyo nayoisemea, hapa nazungumzia blog blog blog. Nikatoa mfano kwamba C.CM wao wana blog ambayo imekusanya hayo yote na web yao pia (au wavuti kama hamkuelewa)
 
Kuna haja ya kutofautisha blog na website/ tovuti na nionavyo mie ni kwamba umeshindwa kuyatofautisha hayo mawili na inawezekana huyaelewi. Nenda kwenye website/ tovuti ya chadema utapata kila kitu ambacho umeshauri kiwekwe. Hapo utakubali kuwa the guys are ahead of you, nenda Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Naifahamu labda uangalie hizi link mbili nazozizungumzia: http://chademablog.blogspot.com/

na ya CCM
[URL]http://4.bp.blogspot.com/-uJTYrX3nV44/T6urqL7VNoI/AAAAAAAAFcQ/Ze4fZmWIgm8/s1600/A13.JPG
[/URL]

 
Back
Top Bottom