Blogs with adsense account

Blogs with adsense account

bongompya

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2015
Posts
224
Reaction score
43
Hello ,
We are here to help you in creating Blog with adsense account with cheapest cost, Please Contact us 0687535650
 
Hello ,
We are here to help you in creating Blog with adsense account with cheapest cost,Please Contact us 0687535650

Kwa msaada wa wengi na kuitangaza vyema biashara yako,hebu elezea hapa hii kitu inakuwaje?na nani amewahi kufanikiwa katika hili,na amefanikiwa vipi?
 
Blogu ni nini?
Blogu ni aina ya tovuti ambayo makala zake hupangwa katika mpangilio unaoanza na makala mpya juu ya ukurasa mkuu (home page) na makala za zamani zikielekea chini. Tofauti kati ya blogu na tovuti za aina nyingine mfano tovuti ya gazeti la mwananchi (tovuti tuli ?static?) au jamii forum (tovuti jukwaa ?forum?) ni hizi zifuatazo.





  1. Maudhui ya blogu (makala, picha, video n.k.)hupangwa kwa kuanza na maudhui mapya yakiwa juu ya ukurasa mkuu halafu maudhui ya zamani yakielekea chini.
  2. Maudhui ya blogu huongezwa mara kwa mara
  3. Wanaotembelea blogu wanaweza kuacha maoni yao kuhusu maudhui au blogu kwa ujumla.
Zipo tofauti nyingine lakini hizi zilizo ainishwa hapo juu kwa pamoja ndiyo zina tofautisha blogu na tovuti nyingine.


Kwa nini watu wanaanzisha blogu?
Watu huanzisha blogu kwa sababu mbali mbali ila kuna sababu ambazo husukuma watu wengi kuanzisha blogu zao binafsi.


Kufundisha; Watu wengi wenye utaalamu au ujuzi na jambo fulani huanzisha blogu kwa ajili ya kufundisha. Mfano mtu anayefanya kazi kwenye duka la kuuzia simu anaweza kuanzisha blogu ya kusaidia watu kutambu simu feki au simu zitakazo kidhi mahitaji au utunzaji bora wa simu yako n.k.
Kusaidia; Kuna watu wanaoanzisha blogu kwa ajili ya kusaidia watu. Mfano daktari anaweza kuanzisha blogu ya kusaidia watu na matatizo yao ya kiafya.


Kipato; Pia wapo watu ambao huanzisha blogu kama njia ya kujipatia kipato. Hapa kuna kuwa na tofauti kati ya blogu moja na nyingine, wapo wanaouza bidhaa kupitia blogu zao, wapo wanaouza ujuzi wao n.k
Hizi ni baadhi ya sababu kubwa zinazo pelekea watu binafsi kuanzisha blogu lakini siyo sababu peke.

Blogging imeanza kuwa kimbilio ya vijana wengi wa kizazi kipya baada ya kugundua Fursa hii ambapo kuna uwezekano mkubwa wa Mtu kujiendeshea Maisha kwa kupitia Hili. Miaka ya nyuma hili halikufikirika kwa Tanzania yetu, ila kwa nchi za wenzetu hasa Ulaya na Africa Magharibi waliliona hili Kitambo.

Miongoni mwa sababu kubwa inayowapelea Watu waanzishe Blogs ni Kujitangaza, Umaarufu zaidi au Kubwa zaidi ni KUPATA PESA. Hapa ndipo Mkazo wangu wa Leo Unaanzia. Kupitia Blogging yako una nafasi ya kujiingizia kipato kizuri tu (Vigezo na Masharti Vikizingatiwa).

Ingawa ukiwa Online na ukaandika aidha kupitia Google kwamba "Making Online" zinaweza kuja address kibao zenye ofa nzuri za kutamanisha lakini nyingi miongoni mwa hizo ni za Uongo, zitakupotezea muda na pengine kukuchukulia hela zako tu. Japo zipo Nyingi, leo naomba nikuambie kuhusiana na Hii Google Adsense, Ambayo kwa Bloggers Wengi ni Mkombozi wa Kweli.

Ni Nini hasa Hii Google Adsense?

Ni Programu inayoendeshwa na Google ambayo humwezesha Mwandishi aliyethibitishwa ambaye yupo katika Network maalum ya Google kuweka Matangazo ambayo hujibadili Automatic Kulingana na Mazingira husika, Matangazo hayo huwa ni katika Mfumo wa Maandishi, Picha, Video au interactive media advertisements ambazo hulenga Makundi Maalum ya Watembeleaji/Hadhira.

Adsense Ina Changamoto nyingi kwa kipindi cha zama hizi ingawa Zipo mbinu zinazoruhisiwa na namna ya kufanya ili Site yako iwe salama na kuingiza Kipato Kizuri zaidi.

Wapo wengi sana wanamefanikiwa na hii kitu ,na mpaka baadhi yao wameweza kuacha hata kazi walizoajiriwa na kuingia zaidi shughuri za blogs na kujipatia kipato kikubwa zaidi.Kama unaitaji maelezo zaidi ni PM .Natumai wengine watachangia zaidi.
Karibu sana.
 
Back
Top Bottom