Blandina Nyoni na uhamisho wa uonevu, na kupendelea kabila lake, marafiki

Huyu mana ningekuwa karibu nae ningejaribu kumuomba tutengeneze kizazi kijacho pamoja.
 

Ww Kabila gani? Nani kukudanganya kuwa Tanzania hakuna Udini? Umesikia maneno ya Jusa baada ya CUF kushindwa Uzini?.....kukudokeza tu kasema, " Cuf imeshindwa kwa sababu JIMBO la Uzini kuna Wakristo wengi na Wabara" hii utaiweka wapi?
Huo Ukabila wa Wachaga na Wapare umeuona wp? Vp kuhusu Wanyakyusa, Vp Wahaya? Na makabila mengine mengi tu yaliyopo hapa nchini! Thibitisha sio unatuhumu tu kwani tunaweza fikiria una Chuki binafsi na hayo makabila. Funguka
 
 
Wanyalukolo mademu kazi yao ni uhausuigeli sasa haya madaraka kawajui wafanyie nini watapuputika wote warudi kuosha vyombo
 
Huyu mama inakula kwake! Mpaka dakika hii hajielewi mambo yanavyomuandama!

Hakuna chochote, hizi tuhuma zipo tu humu JF hazipo TAKUKURU (Uzushi), ni kawaida ya watanzania kulalama tu. Walishasema Serikali haiendeshwi na Mitandao na ususani na mitandao ambayo kutwa inaponda tu Serikali yenyewe na Rais wake.
 

Je mazuri yake unayajua?
 

tofautisha siasa na hali halisi. Udini hutumiwa na wanasiasa kuwaziba baadhi ya watu midomo na kujipatoa kura kipindi cha uchaguzi nothing else. Kuna mapapa na manyangumi wa ukabila tz kumbe na wewe unakubali ukabila upo kwa hayo makabila uliyoyataja. Simaanisi watu wa makabila hayo wote ni walewale, namaanisha baadhi au wengi wao
 
Mbayaaaaaaa hiiii. Dr.Mwita ni RMO hapa Bukoba...........yupo kabisaaaaaaaaaaaaa........tunae jamani tunae.........kumbe alimwamisha kwa zengwe.loh.....Jumatatu nina kikao naye lazima nimtonye anieleze kwa kina.

Mtonye kuhusu Jamii forums kama hajawahi kupita huku,mwambie thread za mbaya wake Nyomi....
 

hii ni point muhimu na nzito sn . Wachaga na wapare wazuia sn rifhiki za watz kuibao
 

kumbe huyu mama ana makubwa ee!
 
Luhanjo, blandina nyoni ahaa kumbe ni wale wale. Dkt marina njelekela nae ni wa huko?
 

Manager mzuri hawezi kusifiwa na wafanyakazi anaowasimamia, na ukiona kinyume chake, hujue hapo hakuna kitu ni kama Pinda tu.
 
Nani wa kumpandisha karandinga? Kikwete? Fredrick warimu? Lowasa? Pinda? Ngeleja? Saidi mwema? Labda kama hakimu atakuwa webb yule refa wa manchester!
 

Mama Nyoni ni JEMBE, aliyafanyia kazi malalamiko yaliyotolewa na mdau hapa JF haraka sana. Kesho yake akamngoa mtuhumiwa, ni mama anayefanya kazi kwa vitendo. Ukitaka ukweli fuatilia nyuzi hapo chini. Acheni majungu bana. Tutaendelea kujibu tuhuma zote za kizushi alizozushiwa mama huyu mchapakazi kwa kadri ya uwezo wetu. Stay tune!

31. Ametengua uteuzi wa Dr Sawa anayesimamia uandikishaji / usajili wa Hospitali binafsi na kumpatia Mtoto wa Balozi Lusinde ambaye ni rafiki yake na walisoma nae High School Kilakala mmoja akiwa Form V mwingine akiwa Form VI

https://www.jamiiforums.com/habari-...dhali-jirekebishe.html?highlight=#post2995740

Re: Dada Dr. Pamela Sawa, tafadhali jirekebishe!


By tutafikatu

N.B: Nimeiweka hapa kwenye siasa, maana Tz kila kitu ni siasa tu!

Nimekuwa na rafiki zangu wazalendo kuliko mimi (kama watatu) ambao wamekutana na mama huyu pale Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Kama kawaida ya mama huyu wote walikuwa wakifika ofisini kwake wanaishia kuondoka wamekwazika, bila kujali malengo yao thabiti ya kuanzisha hospitali na vituo vidogo vya afya nchini Tanzania, kwa lengo la kuboresha maisha ya mtanzania. Hawa ni watanzania ambao wametumia mali zao ili kufungua vituo vya afya nchini, biashara ambayo kwa hakika si ya kuaminika kwa nchi yetu ya Tanzania lakini wakiwa wanaongozwa na dhamira njema ya kusaidia wenzetu nyumbani wamethubutu kujaribu (Mmoja Marekani, mwingine Afrika Kusini, na wa mwisho yupo nyumbani Tanzania). (Tunamshukuru Mungu ndugu zangu hawa wote wamepata usajili baada ya kusota kwa miezi kadhaa wakisubiri kupata usajili).

Naambiwa Dr. Pamella Sawa ni Msajili wa Vituo vya Afya Binafsi na Umma wizara ya Afya. Kitengo ambacho kwa hakika kimekuwa kinazidi kufungia vituo vya watu binafsi kwa maelekezo kwamba havijatimiza vigezo wakati huo huo wakiviacha vituo vya serikali visivyohitajika hata kuwapo kwa jinsi visivyokuwa na sifa za kutoa huduma kwa wananchi.

Kitengo hiki kimekuwa kikipokea rushwa nyingi wawapo kuchunguza utendaji kazi wa vituo vya afya Tanzania, na mara zote wamekuwa wanatengeneza mazingira ya rushwa hata kama huna kosa.

Mtanzania msomi, Dr Pamella anasifika sana kwa kuheshimu raia wa kigeni hususani wahindi wenye vituo vyao vya afya nchini kwetu, huku akiwadharau Watanzania vijana kwa wazee ambao wanajitolea kutoa huduma kama hiyo. Ni mara nyingi utaona mhindi anaruhusiwa kuingia ofisini kwake bila kusubiri foleni ya watanzania waliokaa nje ya ofisi yake.

Ukiingia ofisini kwa Dr. Sawa (Yameshawahi nikuta wakati namsindikiza jamaa yangu kufuatilia usajili wa hospitali yake) utapokelewa kwa moyo mkarimu na wasaidizi wake ambao pia hawaishi kunyanyaswa na dada huyu mrembo lakini ghafla ukashangaa anakutoa kwa ukali kwa kisingizio cha kwamba wana mkutano au subiri mtu mwingine atoke (japo kuna watu zaidi ya watatu wanaotoa huduma katika ofisi yake).

Dr. Sawa anasifika kwa maneno makali ambayo baadhi ya nyakati huleta aibu kwa watanzania wanaoingia ofisini kwake. Watumishi wengi wizara ya afya ambao wanahitaji huduma katika ofisi yake huenda kuongea naye kwa woga mkumbwa utadhani yeye ni Simba, ingawa ana umbile dogo na lenye mvuto.

Wengine wanadai kwamba ati Sawa hutumiwa na baadhi ya rafiki zake kutoruhusu kupitisha maombi ya watu wengine wanaonekana ni hatari kwa vituo vingine vya afya kuendelea kupata wateja (sina uhakika maana maombi hupitishwa na board, ingawa yeye huhusika na hatua zote za kupitia maombi na pia ana nguvu sana kikaoni).

Tunashukuru serikali kutoa fursa sawa kwa wote, maana hata mwanamke msomi kama huyu anaweza kupata nafasi nzuri wizara ya afya makao makuu bila shida yoyote, lakini mambo anayowafanyia watanzania wenye moyo safi wa kutaka kuisaidia jamii yetu yanamfanya aonekane asiyefaa na kwa kweli anatakiwa ajirekebishe haraka.

Kama ni tabia zake za asili basi ajitahidi kuziweka kando pindi awapo kazini.

Lakini Tutafika tu!!!



Mkuu suala hili mfikishie Blandina Nyoni ili amshughulikie huyu dada, maana ameshawashughulikia sana watu kama hawa pale Wizara ya Afya.​
 

You are intoxicated man
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…