WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko, ameziagiza kampuni zote za kuchenjua na kuchoma dhahabu katika wilaya za Songwe, mkoani Songwe na Chunya mkoani Mbeya, kusitisha kwa muda usiojulikana shughuli hizo, baada ya kubaini mchezo mchafu wa utoroshaji dhahabu.
Biteko alisema wachenjuaji hao wameshindwa kutimiza masharti mbalimbali yanayotoa muongozo wa shughuli za uchenjuaji madini na kwamba hatua hiyo itasaidia kukabiliana na wimbi la wizi na ukwepaji kodi.
Waziri Biteko alitoa kauli hiyo hivi karibuni akiwa mkoani Songwe katika ziara yake mbalimbali yanayofanya shughuli za uchimbaji madini na kutoridhirishwa na shughuli hizo na uchenjuaji na kuamuru kusitishwa.
Kufuatia uamuzi huo, wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani Songwe waliiomba serikali kuwaruhusu baadhi ya wachenjuaji na wamiliki waliotimiza masharti, kuendelea na kazi wakidai kuwa kuna kila dalili za wachimbaji wanaoendesha shughuli zao kwa mikopo ya benki kufilisiwa.
Alisema baadhi ya kampuni na watu binafsi wanaofanya shughuli hizo na madini walikopa benki hivyo kusitishwa kwa shughuli hizo kumezuia ulipaji wa madeni na badala yake kumeongeza madeni.
Simon Ndaki, alisema changamoto ya kaboni kwa sasa ni kubwa na kwamba hatua mojawapo kabla ya kutoa dhahabu, watu wanakesha kuzilinda hivyo serikali inapozuia kuendelea na zoezi la kutafuta dhahabu linawakatisha tamaa na kuhofia kupoteza mali dhahabu zao na kukosa fedha.
"Ombi letu sisi wachenjuaji dhahabu na wamiliki wa kampuni za kusafisha dhahabu ni serikali kuruhusu baadhi yetu waliokidhi matakwa ya wizara kuendelea na kazi ili kujiingizia kipato ukilinganisha na ilivyosasa na shughuli zimesimama," alisema Ndaki.
Baada ya maombi hayo, Waziri wa Madini, Biteko, alisema walitoa maagizo hayo kwa sababu ya wachimbaji kutokuwa waaminifu na kwamba baadhi yao wameanza kutuma taarifa kuonyesha hatua walizozichukua hivyo muda sio mrefu baada ya kukamilisha taratibu