Biografia ya mazishi ya hongo

Biografia ya mazishi ya hongo

Naomi Gachanja

New Member
Joined
Sep 14, 2018
Posts
2
Reaction score
1
HONGO.

“Maneno ya kueleza jinsi ulivyokuwa sina. Tunakufahamu kama mwelekezi wa mkoa wetu. maendeleo mengi ya watu teule tumeyaona kupitia kwako. Ulikuwa na bidii za mchwa katika kuwafanya wabunge watetee haki za “wanyonge”. Pale bungeni, wabunge walikuwa katika mstari wa kwaza kuweka mezani yanayotutatiza sisi Watakamore ili wao wateule wapige hatua maishani. Tulikupenda sana lakini kama tunavyofahamu,hukumu hautaepuka. Safiri salama,umsalimu maulana huku nikitumai yakwamba “tutaonana” badaye kwani safari ni ile ile. Leo ni wewe kesho ni mwingine. Langu ni mawili tu. kukuaga kwaheri “ rafiki” wangu mpendwa na kuwapa” mkono” “rafiki” na” jamaa” walioachwa nyuma. Kwa kweli hili "limetuhuzunisha" "mpendwa.” Kutuacha sisi Watakamore ni sherehe kwa masikini kama mie na familia yangu.
 
Kwa heri Hongo hamna aliyedhani kuna siku utakufa,lkn leo ndio hivyo tena umeondoka
 
Back
Top Bottom