Binti wa miaka 12 aliyepata mimba kwa kubakwa, ajifungua

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
DAR ES SALAAM: Binti mwenye umri wa miaka 12 amejikuta akipoteza haki yake ya kuwa mtoto baada ya kubakwa, kupewa ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume.

Ni sawa na kusema mtoto amejifungua mtoto.

Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 inamuelezea mtoto kuwa ni yule aliye na umri chini ya miaka 18 na kimaadili gazeti hili linahifadhi jina lake.

Mwananchi ilienda maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam kumshuhudia mtoto huyo akiwa amempakata mwanae huku akimbembeleza anyonye kwa kuwa alikuwa akilia.

Uso wake uligubikwa na machozi wakati wote wa mazungumzo na gazeti, na unyonge ulizidi pale mtoto wake alipolia. Kilio cha kichanga huyo mwenye umri wa miezi minne, kilitokana na njaa kwa kuwa maziwa ya mama yake yalikuwa hayatoki.

Bibi yake, Elizabeth Mahundi alisema mjukuu wake, alijifungua kwa njia ya kawaida Novemba 28, 2016 katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam.

“Ni kweli kwamba mjukuu wangu ni mtoto wa miaka 12, hakuna aliyeamini kama angeweza kujifungua salama lakini, kwa uwezo wa Mungu, imekuwa. Inahuzunisha, inaumiza naomba Serikali isikae kimya inisaidie,” alisema na kuongeza:

“Akili yake haipo sawa japo alikuwa akisoma darasa la nne Shule ya Msingi Pera, ni mtoto asiyeweza kumhudumia mwanaye. Kila kitu nafanya mimi, na kibaya zaidi sina uwezo kabisa.”

Mtoto huyo alisimulia kinagaubaga alivyofanyiwa ukatili na mwanaume (Jina linahifadhiwa), ambaye anadai ni mtoto wa shangazi yake.

Simulizi ya mtoto

Mtoto huyo alisema, ilikuwa mchana wakati anatoka shule alipokutana na mwanaume huyo ambaye alimvutia kwenye pagale (nyumba mbovu). “Nilikuwa natoka shuleni nikakutana na..., aliniita nikaitika, akanivutia kwenye pagale,” alisema. Alisema mwanaume huyo alimtaka avue nguo lakini kwa sababu hakujua kinachotaka kufanyika, aligoma na kuomba arudi nyumbani.

“Alinikamata akanivua nguo zote na akanifanyia kitu kibaya. Nililia lakini alisema nisimwambie mtu kwani nikifanya hivyo atanifanyia kitu kibaya tena,”alisema.

Mtoto huyo alisema kuwa alirudi nyumbani kwa bibi yake mzaa baba, aliyekuwa akimlea katika kijiji cha Pera, Chalinze, Bagamoyo Mkoa wa Pwani na hakusema kitu akihofia kuumizwa na mbakaji huyo.

“Niliendelea kukaa nikashangaa kila siku nimeshiba, tumbo kubwa ndio wakaniweka kikao nikawaambia ni... alinifanyia kitu kibaya. Wakasema nisiseme kwa mtu,” alisema mtoto huyo na kuangua kilio zaidi.

Mtoto huyo anashindwa kuzungumza kutokana na kilio hicho. Wakati huo mtoto wake aliyekuwa akibembelezwa na bibi alikuwa amelala na hivyo kulazwa kitandani, kwenye chumba kimoja wanamoishi.

Alisema anaomba aendelee na masomo yake kwani anaamini anaweza kumaliza shule.

“Naomba msaada wa maziwa ya mtoto hayatoki na naomba nisome,” alisema.

Hali niliyoikuta nyumbani

Mwananchi lilifika nyumbani kwa familia hiyo na kumkuta akimbembeleza mtoto na ilikuwa kama sinema ya mtoto anayecheza na mdoli wake, akiigiza kumnyonyesha. Lakini hili lilikuwa ni tukio halisi la binti wa miaka 12 akimnyonyesha mtoto wa miezi minne.

“Nyamaza, nyamaza unyonye” ilikuwa sauti ya mtoto huyo akimbembeleza mwanaye.

Bibi Mahundi alisema, mtoto huyo analia njaa. Hata siku Mwananchi linafika katika familia hiyo, inaelezwa kuwa walishindia uji na hali hiyo inasababisha mzazi mtoto akose maziwa.

Hatukuweza kuanza mazungumzo, hivyo ikabidi yatafutwe maziwa kwa ajili ya mtoto.

“Maisha yangu magumu, sina kazi na kama unavyoona. Sina namna inabidi nijitahidi kumlea mjukuu wangu ambaye hajiwezi. Hawezi hata kumfulia mwanae nguo, ama kweli dunia ngumu,”aliongea bibi ambaye alibubujikwa na machozi.

Bibi Mahundi alisema siku hiyo hakukuwa na hata tone la unga.

Afya mtoto huyo imezorota na ngozi yake inaonyesha anakosa lishe bora kutokana na hali ngumu ya maisha inayomkabili bibi yake.

Midomo imebadilika rangi kwa kukosa chakula, ni ukweli usiopingika, anahitaji msaada.

Ilikuwaje

Bibi Mahundi anasema ilikuwa saa sita usiku aliposikia mlango unagongwa. Alifungua na kukutana na mtoto huyo akiwa analia huku akishindwa kuongea.

“Nilishangaa kuona mtoto wangu analia, wakaniambia wameniletea mtoto nimuangalie hali yake, nilichungulia nje na kumkuta akiwa na tumbo kubwa, jasho linamtoka na amechoka sana. Niliishiwa nguvu kwa kweli,” alisema.

Aliwaambia waingie ndani ndipo wakamwambia kuwa mtoto aliyekuwa akiishi Pera, Chalinze kwa bibi yake mzaa baba ameletwa akiwa mjamzito licha ya umri wa miaka 12, alionao.

“Nilimpokea mjukuu wangu, nikalala naye hadi asubuhi. Kulipokucha mama yake alienda kijijini alikokuwa anaishi lakini aliambulia kutukanwa,”alisema na kuongeza:

“Aliambiwa kwanza mtoto si wa kwao kwa sababu kule ni kwa bibi mzaa baba. Na wakajigamba kwamba hakuna sheria inayoweza kuwafanya chochote, kwa unyonge alirudi, nikamsihi atulie tumtunze mtoto tukimuombea uzima.”

Siku ya kujifungua

Baada ya wiki mbili tangu mtoto huyo awasili Dar es Salaam, alipata uchungu. Bibi yake alisema walihangaika kutafuta usafiri hadi Mwananyamala na baada ya muda mfupi, alijifungua kwa njia ya kawaida.

“Nilimshukuru Mungu, sikuamini kama mtoto wa miaka 12 anaweza kujifungua kawaida. Alikaa hospitali siku saba, kisha tukaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na afya njema,”alisema.

Mama yake mdogo, Rose John alisema jambo hilo limeiumiza familia nzima. “Kila nikimuangalia huyo mtoto naishia kulia, natamani kumsaidia lakini hata mie zaidi ya kufanya kazi za ndani sina msaada wowote. Hakika naomba Serikali isikae kimya, huu ni ukatili,”alisema.

Waziri atoa tamko

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema wamepokea kwa masikitiko taarifa hiyo na jitihada zinafanywa kumkamata mwanaume aliyehusika kwenye tukio hilo. “Tutahakikisha kijana aliyempa ujauzito binti huyu anakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya dola,” alisema.

Alisema Serikali haiwezi kuvumilia kuona watoto wadogo wa kike wanadhalilishwa na kupewa ujauzito wakiwa na umri mdogo na hivyo kuacha masomo.

“Hivi kweli tutafikia Tanzania ya viwanda wakati asilimia 27 ya watoto wa kike wanabakwa na kupewa mimba hivyo? Hakika mimba za utotoni na ukatili ni kikwazo,” alisema Ummy. Alisema tayari kikosi kazi kimeanza kufuatilia suala hilo na kuahidi kuwa Serikali itatoa taarifa zaidi ya kitakachoendelea.

Wanaharakati wazungumza

Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, Lilian Liundi alisema lazima ukimya uvunjwe ili hatua za kisheria kwa aliyehusika kumdhalisha mtoto huyo kukamatwa.

“Haijalishi ni binamu, mjomba wala nani anapaswa kukamatwa ili hatua zichukuliwe. Haya masuala ya ndugu ndiyo yaliyotufikisha hapa tulipo kwa watoto wengi kubakwa, kupewa mimba na kuzalishwa kwenye umri mdogo,”alisema.

Mama mzazi azungumza

Mama mzazi wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alisema hana la kuzungumza zaidi ya kuomba msaada kwa ajili ya mwanae.

Kwa atakayeweza kuisaidia chakula anaweza kutuma fedha kwa simu 0787 672117

Chanzo: Mwananchi
 
So Sad!!

Sisi wanaume ni viumbe wa ajabu sana! Mimama imejaa tele mitaani unakwenda kufakamia kitoto cha miaka 12 bora ungebaka hata mbuzi.

Mbaya zaidi mtoto anaishi na bibi yake na matunzo ndio hivyo tena.

Udomo zege na Ushirikina ndio unaleta haya yote.
 
Aiseee... jamaa akamatwe tu coz kamuharibia future binti mdogo sana.
Dah... Ila wakati mwingine sheria haina msaada wa moja kwa moja.... Jamaa akifungwa miaka 30.......huyo mzazi wala mtoto hawana faidika chochote. Kuna haja ya kuziangalia sheria zenye madhara endelevu..
 
Dah... Ila wakati mwingine sheria haina msaada wa moja kwa moja.... Jamaa akifungwa miaka 30.......huyo mzazi wala mtoto hawana faidika chochote. Kuna haja ya kuziangalia sheria zenye madhara endelevu..
Sheria haijakataza binti aliyebakwa kudai fidia ya hela. Huyu binti anaweza kudai fidia ya hela kutoka kwa huyu shetani aliyembaka. Hiyo ni juu ya kifungo cha miaka 30.

Sema watu wengi hawajui haki zao.
 
Oh Lord.! Wangeweka mawasiliano yake ili tumpe msaada hata wa ajira ndogo au mtaji
 
Dohhh wangeweka ht namba ya tigopesa/mpesa tumsaidie mtoto huyu hela ya maziwa kwa kdg kdginasikitisha sana
Mkuu ingia website ya mwananchi hiyo habari ipo na mwishoni wameweka namba ya kumchangia chochote.
 
ukimwi alipimwa?? Mtafuteni na mtuhumiwa wawe wanaenda clinic na mkewe huyo
 
Back
Top Bottom