kanali mstaafu
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 4,318
- 4,098
Nianze kwa kumnukuu SHAABAN ROBERT nguli wa riwaya na ushairi kuwahi kutokea kabla na baadabya uhuru aliyewahi kunena "elimu ni mzigo ambao uzito na thamani yake kamwe haviwezi kujulikana kwa yeyote asiye na elimu".
Elimu ni zaidi ya nyenzo ya kutuzalishia madaktari,waalimu,wahandisi,wanasheriu,wahasibu na wanajimu.elimu ni nyenzo ambayo tukiikazania tunaweza kuvuka hapa tulipo na kupiga hatua nyingine zaidi ya maendeleo ktk nyanja zote.
Lengo za uzi huu ni kuwakumbusha watanzania umuhimu wa elimu kama NYENZO YA KIFIKRA.ukiachilia mbali kutenda,namna jinsi ambavyo mtu anavyoelezea mtazamo wake juu ya kitu fulani utajua tu huyu kiwango chake cha elimu ni duni.mnapaswa mchunguze hasa jinsi watu ambao hawana elimu wanavyowaza kuanzia vyanzo vya mawazo yao mpka ku-connect dots na mpka kuja na misimamo yao.sijaandika huu uzi ili kubeza wale ambao hawakubahatika kupata elimu angalau kufikia ngazi ya shahada bali najaribu kupambanua kwa kina moja ya tatizo ambalo linaitafuna nchi yetu.
Leo asubuhi wakati naelekea kwa Dada wa kinyaturu maarufu kwa upishi wa chapati mujaarabu hapa tabata ili kuweza kufungua kinywa,nilipita katika goli la muuza magazeti nikakuta jamaa wa makamo kama kundi wanabishana juu ya suala la mchanga wa madini (Makinikia).nilisikitika sana baada ya kuwasikia hoja zao na kubwa zaidi ni pale ambapo jamaa aliyeaminiwa kuzungumza kama kinara anasikilizwa na alikuwa amejivika u-much knw (kiredio).nilisikitika sana kuona jinsi gani taifa letu linashindwa kupiga hatua kwa sababu ya kuwa na idadi kubwa ya wananchi ambao hawana upeo wa kuchanganua masuala ya kitaifa na ndio hawahawa wanafnya maamuzi as majority katika kuchagua viongozi wa kiserikali na kitaifa,kushiriki katika vikao vya maendeleo katika mitaa na kata na kuleta misimamo na mitazamo yao ambao inaonekana ni sauti ya watanzania.
Baada ya kukaa na kufikiri kwa kina nimekuja na dondoo fupi ambazo ni sifa za watu wasio na elimu kifikra.
1.wameacha watu wafikirie kwa niaba yao na hivyo wao wamegeuka kuwa wamezaji na wapigia upatu wa kile wanachowaza wanasiasa wanaowaamini
2.wanajiona wanachokijua ni absolutely truth na hakuna ukweli mwingine kwa sababu hicho wanachoona ni ukweli kimesemwa na wanasiasa wanaowaamini
3.hawana muda wa kulinganisha pande mbili yaani mtuhumiwa na anayetuhumu ili kujua ukweli uko wapi
4. Wameshaweka akilini mwao kuwa wazungu ni wezi siku zote na kusahau kuwa hata katika kundi la wakatoliki kuna yule anayekula nyama cku ya ijumaa kuu sasa ili kumbaini lazima tufanye uchunguz
5.wanaona Rais ni Mungu mtu na wengine wanaona viongozi wao wa upinzani ni miungu watu lakini hawafahamu kuwa inaweza kuwa vice versa
6.wana kasumba ya kujiona wanajua kila kitu na mtu anayewa-challenge anaonekana ni mbaya
N.B ....watanzania wenzangu tusipende kuhukumu baada ya kusikia tuhuma bali tutoe uwanja wa kusikiliza pande zote ili tufanye majumuisho ya hoja zao na hapo ukweli utaanikwa peupe mithili ya uchi wa mwandani wako siku ya kwanza ya fungate.
Pongezi zimuendee Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kwa kutupia jicho hili swala na kuwafanya watanzania wajue kuwa hiki kitu kipo.suala la aliyoyasema kuwa ni sahihi au si sahihi tumuache kiranja MUDA ataamua
KANALI MSTAAFU a.k.a MWADHAMA a.k.a MUFTI MKUU