wote mmechangia vyema na inaonyesha mnaifahamu vizuri biharamulo na watu wake, kitu kimoja tu mi nitasema kuhusu biharamulo, halmashauri ya wilaya kuna watu ni kama miungu watu, na wanawatu wao wanaowatumia kwa njia ya kuwapa tenda then wananufaika wote, mji ule barabara zake huwa hazibadiliki na hii ni kwasababu ya kutoa tenda kwa mtu ambae hana hata kifaa kimoja cha kutengeneza barabara, me ninavyojua yeye anagerage ya magari na kuna wakati sijui kama mpaka leo alipata tenda ya kutengeneza magari yote ya halimashauri, jeshi na kadhalika. Pale biharamulo hapawezi kubadilika na hayo majina mliyoyataja yooote ndio BIHARAMULO hakuna mtu wa kufanya kitu pale.