Huu ni Uzi maalum naanzisha ntakua najaribu kushea "vitu vikubwa" ambavyo vimeshawahi kurekodiwa katika sehemu mbali mbali duniani.
Namaanisha vitu ambavyo vimekua vikubwa kuliko kawaida tulivyozoea
Niwe muwazi hii Idea imechochewa (inspired) na kipindi Fulani cha kiteknolojia kutoka channel ya Discovery ambapo wanaongelea "Monster human marvels) kinakwenda kwa jina hilo la heading ya Uzi
Ila tofauti na kipindi hicho hapa ntaongelea Vilivyotengenezwa na binadamu(Man made) na vile vilivyotokea natural pia ntakua nikiweka vitu hivyo " to scale" kulinganisha na vitu vingine
Twende kazi
Pasha Bulker(Meli ya kubwa Tani 76,000 ya kubeba makaa ya mawe) ilivyokwama kwenye tope 2 June 2007, Nobby beach,New Castle, Australia.......Sasa hivi ina jina jipya inaitwa MV Drake
Disclaimer: Hii ni sanamu(replica) ya nyoka walioitwa Titanoboa, kwasasa hawapo(extinct) ila inasemekana waliishi South America huko misituni(Kwenye anaconda) kati ya miaka 58 hadi 60 million iliyopita.
Hii ni pembe ya Mammoth (Sijui Kiswahili?) Ila ni jamii ya tembo. Tuseme ndo babu zao tembo. Waliishi miaka mingi iliyopita. Hii pembe ilipatikana miaka ya 2000 Siberia,Urusi
Huyu jamaa alikua ni msanii wa vichekesho akizunguka na Circus carnivals watu wanamshangaa urefu wake kwa kulipia hela. Wakati wa vita Adolf Hitler akamkamata na kumlazimisha ajiunge na jeshi (Kikosi cha SS)