Biblia aliyotumia Rais Joe Biden Kuapa ina miaka 127!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,433
Wakuu,

Kama tunavyojua tayari Rais wa Marekani ameapishwa na tayari ameanza kazi.

Pamoja na mambo mengine ya kujifunza kwenye tukio la kuapishwa kwake lakini moja wapo ni Biblia aliyotumia kuapa. Rais Joe Biden ni Mkatoliki na anakuwa Rais wa pili Mkatoliki kutawala Marekani baada ya hayati John F Kennedy.

Biblia aliyotumia kuapa ni Biblia ya kifamilia ambayo wamekuwa wakirithishana kwa zaidi ya miaka 127 toka mwaka 1893. Rais Biden ameitumia kuapa pia huko nyuma kwenye nyadhifa tofauti kama picha hii chini inavyoeleza ambayo ni ya mwaka 1973.

Screenshot_20210121-084935_Chrome.jpg
 
Jana nilipoona hii nikakumbuka marehemu babu yangu alikuwa na biblia ya mwaka 1970 ina Kiswahili kitamu sana sijui lahaja gani ile. Baba mdogo aliichukua nitaenda kumuomba anipatie niitunze kwa ajili ya generations kadhaa, sidhani kama aliichukua kama kuitunza bali kuisoma kama zile za sokoni za siku hizi Kiswahili cha mtaani.
 
miaka 127? Ukisoma Biblia kila siku haiwezi kudumu miaka 127. Zaburi 1:1-3
 
Jana nilipoona hii nikakumbuka marehemu babu yangu alikuwa na biblia ya mwaka 1970 ina Kiswahili kitamu sana sijui lahaja gani ile. Baba mdogo aliichukua nitaenda kumuomba anipatie niitunze kwa ajili ya generations kadhaa, sidhani kama aliichukua kama kuitunza bali kuisoma kama zile za sokoni za siku hizi Kiswahili cha mtaani.
Kama kitabu cha sira kipo naitak kwa bei yoyote
 
Hiyo 1973 Joe Biden aliapa akiwa hospitali anauguza watoto wake wawili baada ya ajali ya barabarani iliyochukua uhai wa mke wake na mtoto wake wa kike. Watoto wa kiume 2 walipata majeraha ndiyo mmoja huyo anaonekana

Asante J-Lo.
 
Ingekua huku kwetu, hi ajali ingehusishwa na kafara..., wazungu na sisi nadhani huaga hatupo sayari moja bhana.
 
Back
Top Bottom