Bibi kizee apandishwa kizimbani akidaiwa kuiba gari

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
bibi+pic.jpg

Fatuma Mohammed (70) na Aziz Njakula (36) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya wizi na kupatikana na gari la wizi aina ya Toyota Hiace.

Wakili wa Serikali, Hamisi Said amedai Jumatatu May 15 2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Julai 9, 2015 eneo la Mnazi Mmoja walitenda kosa la wizi wa gari hilo mali ya kampuni ya Choice Motors.

Januari 26, 2016 eneo la Nzasa, Dar es Salaam Mohammed anadaiwa alikutwa akiwa na gari la wizi nyumbani kwake.

Baada ya kusomewa mashtaka washtakiwa wamekana na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika.

Hakimu Simba ametoa masharti ya dhamana kwamba wawe na wadhamini wawili kila mmoja ambao watasaini bondi ya Sh10 milioni. Walikamilisha masharti na kuachiwa kwa dhamana.
 
Hivi mzee wa miaka 70 ataiba gari vipi?
Nitakubali kama alikuwa kwenye gari ilioibiwa hapa inawezekana kaomba apelekwe sehemu. Bahati mbaya kumbe gari lilikuwa la wizi, tunahitaji maelezo ya mtuhumiwa bi Fatima tujue ilikuwaje. Mpaka akawa mtuhumiwa wa wizi wa gari.
Sijui kesi itasomwa lini tena ili tupate 'updates' za wizi huo.
 
Hivi mzee wa miaka 70 ataiba gari vipi?
Nitakubali kama alikuwa kwenye gari ilioibiwa hapa inawezekana kaomba apelekwe sehemu. Bahati mbaya kumbe gari lilikuwa la wizi, tunahitaji maelezo ya mtuhumiwa bi Fatima tujue ilikuwaje. Mpaka akawa mtuhumiwa wa wizi wa gari.
Daah hivyo vi bibi ndio vijizi na vitapeli vikubwa vinaweza vikajifanya vinaomba lifti viko na wajukuu zao,ukawapa lifti kwa kumuonea huruma bibi kumbe hao unaodhani ni wajukui ndio majambazi,mbele mbele wanakutolea bastola,pale mtaa wa jamhuri kuna bibi alimtapeli kaka yangu pesa nyingi sana na mpaka leo hajakamatwa
 
Hivi mzee wa miaka 70 ataiba gari vipi?
Nitakubali kama alikuwa kwenye gari ilioibiwa hapa inawezekana kaomba apelekwe sehemu. Bahati mbaya kumbe gari lilikuwa la wizi, tunahitaji maelezo ya mtuhumiwa bi Fatima tujue ilikuwaje. Mpaka akawa mtuhumiwa wa wizi wa gari.

ACHA PAPARA, NDIO MAANA YUPO MBELE YA MAHAKAMA , UKWELI UTAJULIKANA TU !
 
Hapo rahisi tu huyo ni bibi,utakuta huyo wa miaka36 kaomba ahifadhiwe gari lake,
 
Hivi mzee wa miaka 70 ataiba gari vipi?
Nitakubali kama alikuwa kwenye gari ilioibiwa hapa inawezekana kaomba apelekwe sehemu. Bahati mbaya kumbe gari lilikuwa la wizi, tunahitaji maelezo ya mtuhumiwa bi Fatima tujue ilikuwaje. Mpaka akawa mtuhumiwa wa wizi wa gari.
Labda lilipoibwa likapelekwa nyumbani kwake kuifadhiwa.n.k
Sio wote wanaopanda kizimbani wana hatia.
 
Hivi mzee wa miaka 70 ataiba gari vipi?
Nitakubali kama alikuwa kwenye gari ilioibiwa hapa inawezekana kaomba apelekwe sehemu. Bahati mbaya kumbe gari lilikuwa la wizi, tunahitaji maelezo ya mtuhumiwa bi Fatima tujue ilikuwaje. Mpaka akawa mtuhumiwa wa wizi wa gari.
una uwezo mdogo xn hata wa kuchambua vitu vyepec km hv!
 
Polisi wetu hao....uweledi hawana...upelelezi wao ni wa nguvu tu sio kitaalam ...si mliona jana kosa la parking polisi anapiga risasi itafikiri mwalimu wake ni ISIS
 
Back
Top Bottom