Godee jr
JF-Expert Member
- Apr 17, 2012
- 1,820
- 2,479
Wakuu naandika huu uzi nikiwa na masikitiko makubwa sana. Kama vijana tunajitahidi sana kujiajiri lakini mambo ni magumu sana huku mtaani. Biashara zinazorota sana huku mfumuko wa bei ukiendelea kuwa juu. Juhudi binafsi kwa sisi ambao tumekosa ajira na kuamua kujiajiri zinakatishwa tamaa na huu mzunguko mdogo wa pesa.
Naandika hivi nikiwa ni muathirika mkubwa katika biashara zangu. Ni mwaka jana mwezi wa kumi nilifanikiwa kupata project moja nzuri ambayo ilinipatia pesa kiasi ambazo sikuwahi kuzimiliki binafsi. Nilijitahidi kufungua biashara ya chakula{Majiko katika bar} ili pesa yangu nisiitumie bure. Pamoja na mwanzo mzuri lakini kuanzia January hali illikuwa ngumu sana kiasi cha kujikuta kuwa faida haitoshi tena kulipa posho za wafanyakazi pamoja na kodi na huku kila siku nikipata hasara ya vitu kubaki. Note that hii sio biashara yangu ya kwanza na sio kwamba nilikuwa najaribu biashara no thank you. Mzunguko wa pesa ni mdogo sana. Upatikanaji wa wateja katika maeneo haya umekuwa mdogo sana.
Nashauri pesa zingeachiwa tu katika commercial banks ili tupate mzunguko mzuri wa pesa. Leo hii pamoja na juhudi zangu zote nimekaa kama mgonjwa nikiwaza maisha yanavyozidi kuwa magumu na mbaya zaidi next month land lord anataka bank slip yake.
Mungu tuepushie majanga haya yanayotukabili waja wako.
Hapa kazi tu but work done=ziro