Ruhazwe JR
JF-Expert Member
- Jan 31, 2011
- 3,402
- 944
omba sana mungu uishie kuangalia kwenye move na sio yaje yakupate live hapo ndio utajua dunia kweli inamizunguko miwiliHii sredi nimeivumbua jana make mi si mwenyeji sana JF na nimesoma page zote 1 -25 kusema kweli sina cha kusema ngoja nitafakari angalau wiki nijue pa kuanzia,,, make mimi ni mshabiki mkubwa wa filami za ki Nigeria na kama mnavyojua almost more than 75% ya filamu hizi huonesha mambo ya kishawi,kutokana na fitina, wivu, kutaka utajiri wakatimwingine hata mapenzi na mwisho wake huwa tunaona neno la Mwenyezi mungu linaingilia na kuufunika huo uchawi. kusema kweli hua na nafikiri ni maigizo tu kumbe kuna uhalisia wake sana. kuhusu huyu bwana MAJIMOTO !!!! Duh!!!!!!!!
Mikoa saba nchini Tanzania ndiyo tishio kwa kuwa na nguvu kubwa za uchawi
1. Tanga ndio kinara
2. Lindi unafuatilia
3. Dar es Salaam
4. Mtwara
5. Tabora
6. Kigoma
7. Mwanza
Mikoa yenye wachawi wengi, kwa maana kwamba karibu kila kaya kuna mchawi
1. Sumbawanga (Rukwa) ndio kinara
2. Ruvuma inafuatialia
3. Mbeya
4. Singida
Mikoa ambayo wananchi wake ndio wateja wakuu wa wachawi
1. Kilimanjaro inaongoza
2. Morogoro inafuatilia
3. Kagera
Wateja wengine wa wachawi
1. Wafanyabiashara
2. Wasanii
3. Kina mama wa nyumbani
4. Wanafunzi wa shule za sekondari hasa wa kidato cha pili.
ok,majimoto!kijana anapobaleghe huota njoz za mapenz na kumalza haja zake,the same to girls,kwani hayo ni mabadiliko ya kibaiolojia,inakuaje wengne wananasibisha na MAJINIMAHABA?
Maji moto, swala la ukimwi wa kutupiwa nilishawahi kuona mtu wa aina hiyo lakini baada ya muda alipona na mzima mpaka leo.
Swali- kuna watu wanaishi duniani lakini wana asili ya mizimu walilogwa walipozaliwa au mimba ililogwa hao watu utakuta wanaonekana na watu wachache tu wengine hawawaoni ila wanaishi na wanaendesha maisha yao kama kawaida. inakuwaje hapo?
Kuna watu walikufa zamani lakini bado wapo duniani hii inakuwaje. mimi binafsi kuna mtu alikufa zamani sana mwaka 1994 nikiwa mdogo lakini yupo huwa namuona na anaendesha maisha yake kama kawaida na ni mwanadamu tu kama sisi hii imetokeaje?
Happy new year.
Mkuu majimoto asante kwa ufafanuzi wako. Mkuu majimoto sasa kama unamjua adui yako na kila siku anakufanyia vituko leo hichi kesho kile na unasamehe kila siku kama Mungu alivyosema lakini bado anakuwa kichwa ngumu anaendelea. Sasa Mkuu nitawaitaje Malaika na kuwaambia wakampatie kipigo? Kama wachawi wanakuwa na mikutano yao ya kila siku na wanapangiana kazi za kufanya kwa nini wachawi wa mtaa mmoja wanauana?
Mkuu kuna testimony nyingi za watu wanaosema kwama walipelekwa Jehanam na Yesu na wakaona watu wakipata mateso yasiyokifani sasa hawa ni waongo ama kuna sehemu nyingine ambayo watendeji dhambi wanapelekwa kabla ya Jehanam na ambao hawana dhambi wanaenda wapi?
Hayo Joyceline aliongelea yameshamtokea rafiki yangu mmoja nilipokuwa mdogo alikuwa anatuambia anakuja kuchukuliwa shuleni na kurudishwa nyumbani na mmoja wa rafiki za mama yake ambaye alikuwa ameshafariki.Siku moja mama yake akamuuliza unarudishwa na nani nyumbani, akamwambia ni yule rafiki yako wa pale madukani mama yake akamwambia yule mama alishafariki siku nyingi lakini binti alibisha sana ikabidi siku hiyo mama yake aje shuleni kumchukua ili aone kama atakutana na huyo rafiki yake lakini hakumuona na wala huyo rafiki yake hakutokea mpaka hivi leo. Ina maana misukule wanaendelea kusaidia watu wanaowajua kama wakikutana nao? Ama alikuwa anampangia nini huyo mtoto?
Kuzimu ni sebule (sitting room) ya shetani, watu wote wanaokufa wakiwa wateja wa shetani hukaa mkono wa kuume wa shetani ndani ya sebule yake. Shetani anawatumikisha apendavyo, kwa suluba na vipigo vya kutisha, kimsingi mtu yeyote anayekufa, kinachokufa ni mwili wake, endapo utaingia kuzimu, kifo chako cha pili cha roho yako ni lazima, siku ya siku ikifika roho yako itaondolewa kuzimu na kutupwa jehanam na hiyo ndiyo itakuwa mauti yako ya pili.
Watu waliopelekwa kuzimu wanaweza kabisa kutolewa na kurudi tena duniani.
Maduka mengi katika jiji la Dsm yanaendeshwa kwa juju. Usishangae mwanao aliyekufa siku chache zilizopita yuko ndani ya nyumba ya jirani yako au ndugu yako akitumikishwa. Jambo moja ambalo napenda kulisema tena, hakuna kijana yeyote aliyekufa ghafula kwa ugonjwa au kwa ajali na kuzikwa, mwili wake ukabaki ndani ya kaburi, hakuna. Lipo andiko langu nilisema tekinologia yote inayotumika sasa hivi duniani chanzo chake ni kuzimu, nitaelezea hili siku nyingine. Vijana wenye nguvu na walioelimika wanatafutwa kama dhahabu ya mwadui huko kuzimu na vifo vya ghafula huhamisha mamia ya hawa vijana kila mwaka toka maisha ya kidunia na kuwashusha kuzimu kutumikishwa.
Bwana Majimoto naona hii ni imani nyingine unayoileta hapa, uchawi, shetani, mapepo, majini, nk hivi vipo lakini unapoingiza swala la wafu na hali zao naona unajichanganya maana ki Kristo wafu wako katika makaburi yao, wala hawamkumbuki Mungu, hawamshukuru, au kumsifu(zaburi 6:4-5, zaburi 115:17) kwa sababu hata mawazo yao yamepotea (zaburi 146:3-4). Walio hai ndio wanojua kuwa watakufa lakini wafu hawajui neno lolote, kumbukumbu lao limesahauliwa, kifo hufananishwa na usingizi (zaburi 13:3), (Ayubu 14:10-12). Yesu aliweka bayana alipomzungumzia Lazaro (Yohana 11:13-15). Hata hivyo biblia inaongelea kufufuliwa kwa waliolala wengine kwa maisha ya milele wengine kwa mauti ya milele (Daniel 12:2, Yohana 5:28-29, Ufunuo 20:14)Kuzimu ni sebule (sitting room) ya shetani, watu wote wanaokufa wakiwa wateja wa shetani hukaa mkono wa kuume wa shetani ndani ya sebule yake. Shetani anawatumikisha apendavyo, kwa suluba na vipigo vya kutisha, kimsingi mtu yeyote anayekufa, kinachokufa ni mwili wake, endapo utaingia kuzimu, kifo chako cha pili cha roho yako ni lazima, siku ya siku ikifika roho yako itaondolewa kuzimu na kutupwa jehanam na hiyo ndiyo itakuwa mauti yako ya pili.
Bwana Majimoto naona hii ni imani nyingine unayoileta hapa, uchawi, shetani, mapepo, majini, nk hivi vipo lakini unapoingiza swala la wafu na hali zao naona unajichanganya maana ki Kristo wafu wako katika makaburi yao, wala hawamkumbuki Mungu, hawamshukuru, au kumsifu(zaburi 6:4-5, zaburi 115:17) kwa sababu hata mawazo yao yamepotea (zaburi 146:3-4). Walio hai ndio wanojua kuwa watakufa lakini wafu hawajui neno lolote, kumbukumbu lao limesahauliwa, kifo hufananishwa na usingizi (zaburi 13:3), (Ayubu 14:10-12). Yesu aliweka bayana alipomzungumzia Lazaro (Yohana 11:13-15). Hata hivyo biblia inaongelea kufufuliwa kwa waliolala wengine kwa maisha ya milele wengine kwa mauti ya milele (Daniel 12:2, Yohana 5:28-29, Ufunuo 20:14)
Kama ni elimu mpya tofauti na hii ya Kikristo (maana hata signature yako inathibitisha wewe ni mkristo) tuambie mapema kuliko kuelekea kusiko na kupoteza wengi wenye ufahamu kidogo juu ya hali ya wafu.