Biashara ya kutotoa na kuuza vifaranga

Biashara ya kutotoa na kuuza vifaranga

Status
Not open for further replies.

Biashara2000

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2013
Posts
624
Reaction score
548
Habari. Egg incubators za size mbalimbali zimekuwa zikitumiwa na wafugaji nchini kutotolea vifaranga kwa ajili ya ufugaji binafsi. Ila ni watu wachache tu ndio wamekuwa wakitumia incubator hizi kutotoa vifaranga na Kuuza kibiashara.

Na hawa hutumia incubator za millions ambapo vijana na wajasirianali wadogo hawana hizo millions ili nao waanzishe biashara hizo. Sasa habari njema ni kuwa hata ukiwa na mtaji wa wastani unaweza ingiza kipato cha sh. 390,000 kila baada ya siku 21.

Unahitaji kuwa na mtaji wa sh.750,000. Km eneo la kuendeshea mradi huu unalo inakuwa rahisi zaidi. Katika kiwango hicho unahitaji incubator ya umeme yenye uwezo wa kutotolesha mayai 300 kuwa vifaranga. Gharama ya incubator ni sh. 400,000, unahitaji generator sh. 300,000 na sh. 50,000 ya kununulia mayai na umeme wa kuanzia.

Utakuwa na uwezo wa kutotoa vifaranga 300 kwa siku 21 na iwapo ukiuza kifaranga kimoja bei ya sasa ya sh. 1,300 utapata sh. 390,000. Kwa mantiki hiyo katika siku 42 Utakuwa umepata sh. 780,000 hivyo mtaji wako unakuwa umerudi katika siku hizo.

Unaweza tumia incubator za kerosene ila zile hazigeuzi mayai automatic hivyo ni lazima uwepo pembeni yake na usiende shughuli zingine. Pia usipokuwa mwangalifu madhara yanaweza kuwa mengi kerosene ndani nyumba. Hii ya kwetu inageuza mayai yenyewe hivyo huna haja ya kuwepo karibu muda wote. Kwa incubator hii unaweza totolesha mayai ya aina mbali mbali za ndege. Ntaweka picha soon.
 
Sijaelewa hapo kwenye generator mkuu. Maana umesema ni ya umeme
 
Umeme wa Tanzania sio wa uhakika. Tanesco wakichukua umeme hata kwa muda mfupi mayai hayatpi vifaranga.


Tunaweza kukutengenezea ya sola ila ni expensive. Kwa 900, 000 utapata ya mayai150
 
Umeme wa Tanzania sio wa uhakika. Tanesco wakichukua umeme hata kwa muda mfupi mayai hayatpi vifaranga.


Tunaweza kukutengenezea ya sola ila ni expensive. Kwa 900, 000 utapata ya mayai150
Nahitaji incubator ya mayai 600 mtanitengenezea kwa bei gani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom