Biashara ya kukopesha pesa, njia mpya ya utakatishaji pesa

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Asante ndugu na jamaa wote, kuna jambo moja napenda kuliweka mbele yenu

Kumeibuka na watu binafsi au kikundi kinachofanya biashara ya ukopeshaji pesa

1: Hawajasajiliwa na serikali
2: Serikali haipati kodi wala faida yoyote
3: Wanatakatisha pesa maana wengine wanatumika kusambaza pesa haramu za wizi na kuwakopesha watu kuzihalalisha
4: Ina masharti ya unyonyaji na ovyo

NB: Naomba serikali itazame watu hawa wanaoendesha shughuli ya ukopeshaji pesa
 
Ukitaka kuokoa taifa kuwa muwazi, ni wapi zoez hilo linafanyika na terms zao za mikopo. Ikibidi uambatanishe na document yoyote ili tupate pa kuanzia. U too general boss.
 
Ukopeshaji wa hela ulikuwepo kabla uhuru na ndio njia ya kusaidiana matatizo...hivi mleta mada pata picha mtu mtoto kaishiwa damu au ugonjwa wowote ule na hospital hazina huruma huna hela mtu anakufa, na unakuta jiran yako anakopesha laki moja kwa liba ya elf 20 kwa mwezi hivi uache kwenda chukua hela kama hiyo eti usubiri uende bank kwa loan officers ambao watataka
1. Barua toka kwa mwajri wako
2. Salary slip za miez 5 respectively
3. Ujaze fom zao za mkopo
Then usubiri miezi 3 had 6 ndo uingiziwe hiyo hela,
Hii bsness inaokoaga vitu vingi sana haina haja ya kupiga porojo hizi
 
Acha wivu shida zako ndio zimekupeleka, kwan lazima uende kwao si uende bank ukakope kama wana mashart mepesi.
 
ni kweli kuna jamaa yangu juzi ameenda kukopa hela kapewa hela mabunda tayari yana ukungu.....anakwambia uyo jamaa hata uende na shida ya sh ngapi anakupa tu hana shida.
 
Asante ndugu na jamaa wote, kuna jambo moja napenda kuliweka mbele yenu

Kumeibuka na watu binafsi au kikundi kinachofanya biashara ya ukopeshaji pesa

1: Hawajasajiliwa na serikali
2: Serikali haipati kodi wala faida yoyote
3: Wanatakatisha pesa maana wengine wanatumika kusambaza pesa haramu za wizi na kuwakopesha watu kuzihalalisha
4: Ina masharti ya unyonyaji na ovyo

NB: Naomba serikali itazame watu hawa wanaoendesha shughuli ya ukopeshaji pesa
Kwani ulilazimishwa kukopa?
 
Back
Top Bottom