wanapatikana kwa kiwango cha mpaka kuexport kweli?...mi naona hawatoshelezi hata mahitaji ya ndani, kama unajua pa kuwapata kwa wingi unaweza kuchukua tender hata mahotelini tu ukapata faida nzuri, biashara ikishasimama na ukawa na uzoefu nayo inakuwa rahisi zaidi kwako kuexport.
hao wanakujua walikuwa wanakutengeneza wakupige tu, kama una shida na aina zote za kamba na samaki wengine si unaanzia ferry? na soko si unatafuta kwa walaji wakubwa? na unalipa pesa unapewa samaki unaondoka zako?Hii biashara bwana..kuna jamaa alinipigia simu ya kutaka kunitapeli eti tufanye hii biashara..akanipa namba ya mzee anayevua hao samaki niongee nae kuhusu kupata mzigo,nikampigia kwa namba tofauti akajichanganya mwenyewe..nikamwambia tafuta njia nyingine ya kupata hela hii imebaunsi Bro..
Habari za asubuhi ndugu zangu.
Hongereni kwa kazi na majukumu ya kila siku, Moja ya shauku yangu ya siku nyingi sana ni kusafirisha samaki aina ya kambakochi kwenda China maana ndio soko na uhitaji mkubwa wa kamba kochi ulipo.
Hivyo basi kwa neema ya Mungu natarajia kuanza kupeleka samaki hao mwezi wa nne mwaka huu, na nimeanza kufanya utafiti wa upatikanaji wake pamoja na bei zake pale Feri, na nimefahamu kuwa kilo moja ya kamba aliye hai ni elfu tisini na aliyekufa ni elfu thelathini.
Biashara hii mimi sijawahi fanya wala sina uzoefu nayo. Hivyo kukiwa kuna yeyote anaifanya biashara hii au anaufahamu wa namna moja au nyingine kuhusiana na biashara hii ya kambakochi, naomba mchango wenu katika hili kupitia habari hii ili wengi wanufaike ili nao wapate kuona fursa na kuchukua hatua ya mafanikio.
Asanteni sana, karibuni sana.
China wanauzwaje!!!!?
Sawasawa wewe unafanya hii biashara au!!!?
Kwanini uliachana nayo? , naomba unipe uzoefu wako wa hii biashara A to Z!!!
Kwanini uliachana nayo? , naomba unipe uzoefu wako wa hii biashara A to Z!!!
English name: Lobster, ni kwa ajiri ya kula!!!