@Fuso,
nashukuru kwa hiyo changamoto.
Kilichonisukuma kupata wazo hili ni mapungufu ambayo nimeweza kuyaona katika centers na hata vyuo vinavyotoa hizi short courses . Wengi hawafundishi vizuri, siku zingine hakuna walimu, kozi huchukua muda mrefu bila sababu , practice kwa wanafunzi ni kidogo. Siku si nyingi nilimpeleka mtu chuo kilichosajiliwa veta asome ms publisher, hali halisi ni kuwa darasa lina wanafunzi wengi na anaelekezwa na mwalimu si zaidi ya dakika kumi kati ya masaa mawili ya siku.