Hapa na type nikiwa Comoros; ni siku ya 10 toka nifike huku.
Nimesoma comment za uzi wako zote na maswali yako nimeyaona.
Kwa ufupi niseme Comoro pesa ipo na kea huo mtaji wako kama ukipata mwongozo sahihi Faida ipo; ila shida inakuja kuwa ni nani atakupa huo mwongozo?
Ukisema uke kufanya tafiti, huo mtaji wako utaishia kwenye utafiti na unaweza ukaishia airport ana jela.
Kama ukiamua kuja gharama ni kama zifuatazo:
1. Visa 125,000
2. Nauli ya Ndege ni kuanzia 1100,000 na kuendelea
3. Guest bei ya chini ni elf 50 kwa siku.
4. Chakula mlo moja ni kuanzia elf20
Kwa hiyo ukiangalia hayo mahesabu utagundua katibia nusu ya mtaji wako unakatika hapo.
Maelezo zaidi utayapa kwenye uzi wangu kuhusu safari yangu ya baada ya kurudi nitaweka kila kitu humo isipokuwa connections tu